“We live in the age of philosophy, science, and intellect. Huge libraries are open for everyone. Everywhere we have schools, colleges, and universities which give us the wisdom of the people from many previous millennia. And what then? Have we become wiser for all this? Do we better understand our life, or the meaning of our existence? Do we know what is good for our life?” — JEAN JACQUES ROUSSEAU
Tunaishi kwenye zama za taarifa,
Katika zama hizi upatikanaji wa taatifa na maarifa ni kitu rahisi kwa kila mtu.
Kwa kutumia simu yako janja, una uwezo wa kupata taarifa na maarifa mengi sawasawa na mtu yeyote yule duniani kwa sasa.
Una uwezo wa kupata taarifa na maarifa mengi kuliko watu wote walioishi miaka 50 iliyopita.
Maarifa ni mengi mno, na rahisi sana kwako kuyapata.
Lakini swali ni moja, maarifa hayo yamekusaidiaje?
Ni vitu gani umeshajifunza na kuvifanyia kazi kwenye maisha yako kiasi cha kuwa tayari kujivunia kupata maarifa hayo?
Kwa wengi, maarifa wanayaacha yaelee huko mtandaoni,
Hawachukui muda kujifunza na kuyachakata maarifa hayo ili yawe na manufaa kwao.
Wanschojiambia ni wakitaka kujua kitu wata google, hivyo hakuna haja ya kujifunza maarifa mengi.
Huko ni kujidanganya na usikubali kuingia kwenye mkumbo huo.
Maarifa unayoyapata kwa kutafuta mtandaoni ukiwa na uhitaji huwa hayana manufaa kwako.
Maarifa yanayokuwa na manufaa ni yale unayojifunza kwa kina, ukayatafakari, ukayachakata, ukaunganisha na maarifa mengine uliyonayo, kisha ukaangalia hali unayokabiliana nayo na kisha kufanya maamuzi sahihi.
Usifurahie kuwa na simu janja kwa ajili ya kufuatilia maisha ya wengine na habari mbalimbali.
Bali furahia kuwa na simu hiyo kama fursa kwako kujifunza mambo kwa kina.
Kisha kila siku tenga muda wa kujifunza vitu kwa kina na kuvitafakari kwa namna ambayo vitakuwa bora zaidi kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kelele na kazi kutokwenda pamoja, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/08/2016
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,