“There is only one time that is important – Now! It is the most important time because it is the only time when we have any power.” — Leo Tolstoy

Muda wa kipekee kwako ni sasa,
Muda ulionao sasa ndiyo muda muhimu zaidi kwako,
Ndiyo muda ambao una nguvu ya kuutumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Lakini umekuwa hutumii muda huo, badals yake unaupoteza.
Umekuwa unaupoteza kwa kufikiris yaliyopita, ambayo huna uwezo wa kuyabadili.
Kama hiyo haitoshi pia umekuwa unafikiria yanayokuja, ambayo bado hujayafikia hivyo huna cha kufanya.
Njia pekee ya kupiga hatua kwenye maisha yako, ni kutumia muda ulio nao sasa.
Fanya kile kilochopo mbele yako kwa wakati huo,
Na mawazo yako yote yaweke kwenye kile unachofanya.
Pale unakopeleka fikra zako, ndipo nguvu zako zilipo.
Unapotawanya fikra zako, unatawanya na nguvu zako pia.
Na nguvu zilizotawanyika, haziwezi kufanya makubwa.

Kuna mengi yanawinda umakini wako,
Yanataka utawanye nguvu zako,
Yatambue na sema hapana,
Peleka nguvu zako kwenye kile muhimu unachotaka kufanya,
Na ukishakimaliza unaweza kwenda kwenye kingine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu urahisi na raha ya kufanya, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/09/2017-urahisi-na-raha-ya-kufanya/

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,