Marcus Aurelius wanted us “to bear in mind constantly that all of this has happened before. And will happen again—the same plot from beginning to end, the identical staging.”

Kila kinachotokea sasa, kilishatokea tena huko nyuma.
Hakuna kitu kipya kinachotokea hapa duniani.
Mambo ni yake yake, yanajirudia kwa sura tofauti.
Kumekuwa na majanga mbalimbali yanayojirudia duniani, kuanzia milipuko ya magonjwa na hata manadiliko ya kimazingira.
Dunia imepitia vita, tawala za kimabavu na ukatili wa kila aina.
Mambo hayo yalitokea, yanatokea na yataendelea kutokea.

Uzuri ni kwamba pamoja na magumu mengi ambayo tumepitia, sisi binadamu tumekuwa tunayavuka na kizazi chetu kuendelea,
Japo wengi waliondolewa na majanga hayo, bado wengine wamebaki na kizazi cha binadamu kuendelea.
Hivyo kwa kuangalia yale ambayo yamekuwa yanatokea kipindi cha nyuma, tunaweza kuona kwamba haijalishi tunapitia nini, tutaweza kuvuka na kuendelea na maisha.
Tunaweza kuona kwamba hakuna tukio moja tunaloweza kusema ndiyo mwisho wa wote.

Lakini tuna tatizo moja, huwa hatujifunzi kutoka kwenye historia.
Maana tumekuwa tunarudia makosa yale yale yaliyofanywa na waliotutangulia pale walipokabiliana na hali mbalimbali.
Kama tungekuwa tunajifunza kupitis historia, na kuangalia hatua walizochukua wengine, zipi sahihi na zipi siyo sahihi,
Tungeweza kupunguza changamoto nyingi.
Lakini hatujifunzi, tunarudia makosa yale yale na hivyo kufanya changamoto zichukue muda zaidi.

Tuchukue hatua ya kujifunza kupitia historia na wengine.
Chochote unachopitia sasa, hata kwenye maisha yako binafsi,
Kuna wengine walishakipitia, wakakitatua na kwa bahati nzuri wakaandika kitabu kuelezea jinsi walivyotatua.
Sasa ya nini wewe kuteseka kujaribu vitu vinavyoendelea kushindwa wakati njia ya uhakika ipo?
Kabla hujaendelea kupambana na hali yako, hebu tafuta kwanza waliopambana na hali kama yako na wakafanikiwa, kisha soms kile walichoandika au kilichoandikwa kuhusu wao na ujue hatua sahihi za kuchukua.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu sifa za kuangalia kwa mtu wa kushirikiana naye, fungua; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/11/2019

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,