“Talent is insignificant. I know a lot of talented ruins. Beyond talent lie all the usual words: discipline, love, luck, but, most of all, endurance.” — James Baldwin
Mafanikio yanahitaji zaidi ya kipaji,
Wengi hufikiri kwa kuwa na kipaji fulani inatosha kufanikiwa.
Lakini kipaji pekee hakikufikishi popote,
Wapo wenye vipaji wengi lakini hakuna kikubwa wamefanya.
Mafanikio yanahitaji vitu vingi, lakini vya msingi kabisa ni!
Kazi, lazima uweke kazi ya kutosha.
Nidhamu, unahitaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu sana kwenye maisha yako.
Upendo, kujipenda mwenyewe, kuwapenda wengine na kupenda unachofanya ni hitaji muhimu kwenye mafanikio.
Bahati, ndiyo, kuna bahati utakutana nazo, ambazo zitakusaidia kufika unakotaka kufika. Ila bahati hizo hazitakufuata ukiwa umelala, utakutana nazo ukiweka kazi.
Uvumilivu, hakuna chochote kitakachokwenda ulivyopanga, safari ya mafanikio haitakuwa rahisi, utakutana na magumu na vikwazo na uvumilivu pekee utakaokufanya uendelee na safari hii.
Hayo ndiyo ya msingi kabisa, lazima uyaishi kila siku kwenye kila eneo la maisha yako unalotaka kufikia mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu hakuna anayejua anachofanya, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/20/2028
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Hakika asante Sana kocha kocha, nidhamu ni muhimu sana kwa kila Eneo la maisha yetu ni huanguka hapo kwa kukosa nidhamu binafsi, nidhamu katika kazi,nidhamu ya pesa,
LikeLike