“Forgiveness is not forgetting. Forgiveness is freedom from hate.” — Valarie Kaur

Msamaha siyo kusahau kile ambacho mtu amekufanyia,
Bali msamaha ni uhuru kutoka kwenye chuki,
Unaposamehe, unajiweka huru,
Usiposamehe unakuwa umejiweka kwenye kifungo cha chuki ambayo itaendelea kukutesa.
Hivyo usikubali kukaa na chuki au vinyongo vya aina yoyote.
Samehe kila aliyekukosea au kukukwaza,
Siyo kwa sababu yao, bali kwa sababu yako binafsi.
Hata kama hajaomba msamaha, wewe samehe,
Itakupa utulivu mku wa wa ndani.
Haijalishi mtu amefanya jambo la aina gani,
Unapaswa kusamehe.
Kutokusamehe ni sawa na kuwa na kidonda, halafu kila siku unakitonesha, hakiwezi kupona kamwe.
Samehe kwa sababu unataka kuwa huru,
Hiyo ni adhabu tosha kwa wale wanaokukosea au kukifanyia mabaya.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu tofauti ya mjasiriamali na mfanyabiashara, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/28/2036

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,