“To be what we are, and to become what we are capable of becoming, is the only end of life.” — Robert Louis Stevenson
Lengo kuu la maisha, kusudi pekee unalopaswa kuliishi ni kuwa wewe, kuweza kufikia uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
Hakuna mwingine kama wewe hapa duniani, hajawahi kuwepo na hatakuja kutokea.
Una utofauti na upekee mkubwa,
Una uwezo wa kufanya vitu ambavyo hakuna mwingine anayeweza kufanya.
Uwezo huo umezaliwa nao na ukachochewa zaidi na mazingira uliyopitia.
Lakini hakuna anayejua uwezo wako mkubwa,
Na jamii haiwezi kukusaidia kujua na kufikia uwezo huo.
Kitu kikubwa jamii imeweza kufanya ni kukufundisha kufanana na wengine.
Ndiyo maana shuleni wote mlifundishwa sawa na kupewa mtihani wa aina moja.
Na kwenye maisha jamii inakulinganisha na wengine.
Kutokana na nguvu hii kubwa ya jamii, tumekuwa tunakimbizana na yale jamii inatupa,
Ni mpaka tunapofika mwisho ndiyo tunagundua hakikuwa kitu sahihi,
Licha ya kupata kila ambacho jamii imetuambia ndiyo mafanikio na maisha mazuri,
Ndani yetu bado tunakuwa na utupu,
Tunaona maisha yetu bado hayajakamilika.
Ni wakati sasa wa kukaa chini na kuisikiliza nafsi yako,
Kwa sababu inajua kile unachotaka, inajua uwezo mkubwa ulio ndani yako.
Haijalishi umepotea kiasi gani,
Wakati wowote unaweza kuanza kuitafuta njia sahihi.
Kitu cha kwanza kufanya unapojua umepotea, ni kuacha kuongeza mbio.
Wengi wanapogundua wamepotea, hukazana kuongeza mbio, kitu kinachowapoteza zaidi.
Isikilize nafsi yako,
Tambua uwezo mkubwa uliopo ndani yako,
Na kazana kuufikia huo,
Hilo ndiyo litaleta maisha kamilifu kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kunusa hatari, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/29/2037
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
Asante Sana kocha,juzi kaja tena Yule mtu wa Qnet ,nikamkatalia maana kila siku ananisumbua na biashara yao hiyo ya Qnet, nitajitaid muda wote kuwa mimi sio yule.
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike
Hiz Qnet nao bhana wanasumbua…….kweli kabisa kuangalia jamii kile wanachothaminisha kuwa ukiwa navyo ndo mtu wa maana unapoteza….iweje ramani ya maisha yako richie wewe wengine wakusomee…
Hakuna anaejua zaidi yako mwenyewe
LikeLike
Kabisa.
LikeLike