“Take a simple idea and take it seriously.” —Charlie Munger

Kila mtu anataka mafanikio makubwa, ila wanaoyapata ni wachache sana.
Siyo kwa sababu wachache hao ni wajanja sana au wanafanya nakubwa sana.
Bali kwa sababu wachache hao huwa wanakuwa tayari kukomaa na kitu mpaka wapate majibu.

Wale wanaofanikiwa sana, huwa wanachukua kitu cha kawaida na kukomaa nacho mpaka kiwape matokeo wanayotaka.
Wanaweka umakini wao kwenye kitu hicho na hawayumbishwi na chochote.
Hilo linajijenga na baadaye kuwa mafanikio makubwa.

Wale wasiofanikiwa huwa hawakomai na kitu kwa muda mrefu.
Huwa wanaanza vitu vipya wakiwa na moto kweli kweli,
Lakini siku chache baadaye moto huo unazima na wanaacha kujisukuma.

Kitu kimoja unachoweza kujijengea ili kufanikiwa ni hicho,
Chagua kitu na komaa nacho mpaka upate matokeo makubwa.
Mfano;
👉🏽Kwenye akiba, chagua kuweka akiba ya asilimia 10 ya kila kipato chako bila kuacha, kisha wekeza akiba hiyo.
👉🏽Kwenye kujifunza chagua kusoma kurasa 10 tu za kitabu kila siku bila kuacha hata siku moja.
👉🏽Kwenye uandishi chagua kuandika maneno 500 tu kila siku bila kuacha hata siku moja.

Fanya hivyo pia kwenye kazi, biashara, mahusiano na maeneo mengine ya maendeleo binafsi.
Kwa msimamo wako wa kufanya bila kuacha, utafikia mafanikio makubwa.

NidhamuUadilifuKujituma

AfyaUtajiriHekima

KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa leo ni kuhusu kuweka wazi misingi yako ya kibiashara, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/07/31/2038

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.