“The worst punishment is the understanding that you failed to properly use those good things which were given to you. Do not expect a big punishment. There can be no harder punishment than this remorse.” – Leo Tolstoy
Adhabu kubwa kabisa utakayoipata kwenye maisha yako ni kujua kuna vitu ungeweza kuvifanya, lakini hukuvifanya.
Kwa maneno mengine, majuto.
Majuto yatakuumiza sana wewe mwenyewe.
Kwa kuwa unajua kabisa ilikuwa ndani ya uwezo wako, uliiona kabisa fursa, lakini hukufanya.
Ubaya ni kwamba, wakati unajutia hutazikumbuka zile sababu ulizojipa ili kuacha kufanya,
Badala yake utakumbuka kwamba hukufanya,
Na hilo litakuwinda na kukunyima utulivu maisha yako yote.
Kwa kila muhimu unachopanga kufanya au unachojua unapaswa kufanya, lakini hukifanyi, pata picha ni miaka 10 imepita na huna tena uwezo wa kukifanya.
Ona ni kwa kiasi gani utajutia.
Sasa unayo nafasi ya kuzuia majuto hayo, kwa kufanya sasa kile unachojua unapaswa kufanya.
Waswahili wanasema majuto ni mjukuu, kwamba yanakuja baadaye.
Wewe huna haja ya kusubiri mpaka yaje, maana mpaka yanakuwa majuto, huwezi tena kufanya.
Jiwekee msingi huu kwenye maisha yako, kuishi kwa namna ambayo hutajutia chochote kwenye maisha yako.
Hiyo itamaanisha kujisukuma zaidi sasa,
Lakini baadaye itakupa utulivu mkubwa.
Maana utajua ulifanya kila ulichoweza na ulichopaswa, hata kama matokeo siyo uliyotegemea, kitendo cha kufanya, kitakuridhisha sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu hitaji la watu kuamini, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/03/2042
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.
Ahsante sana kocha.
LikeLike