“What you do, you possess. You must believe that eternal goodness exists that is within you, and that it grows and develops as long as you live.” —Ralph Waldo Emerson
Unakuwa kile unachofanya, na siyo unachotamani kuwa.
Ukifanya mema unakuwa mwema, ukifanya mabaya unakuwa mbaya.
Huwezi kuwalazimisha watu wakuone unavyotaka wewe,
Bali wao wenyewe watakuona kwa yale unayofanya.
Hivyo badala ya kuhangaika kushawishi watu wakuoneje, hangaika kufanya kile ambacho unataka kuwa.
Kupanga ni rahisi, kuongea ni rahisi, lakini kufanya ni ngumu.
Ndiyo maana wengi ni wapangaji na waongeaji, ila watendaji ni wachache sana.
Watendaji wanaaminika na kupewa nafasi kubwa na nzuri zaidi.
Kuwa mtendaji na utakuwa kile unachofanya.
Kila unachotaka tayari kipo ndani yako, kinasubiri wewe uanze kuchukua hatua, kijengeke na kukupa matokeo sahihi.
Hivyo kuwa mtu wa kuchukua hatua.
Pia kuwa na subira, matokeo hayatakuja haraka kama unavyotaka, hasa kwa mambo makubwa.
Wajibu wako ni kufanya na matokeo yatakuja kwa wakati wake.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu usihangaike kuibadili dunia, bali badili hiki kimoja na dunia itabadilika, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/10/2049
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.