“Do not be interested in the quantity of people who respect and admire you, but in their quality. If bad people dislike you, so much the better.” —Lucius Annaeus Seneca

Kwenye maisha yako, usisumbuke na wingi wa watu wanaokukubali, wingi wa marafiki au wingi wa wateja.
Badala yake kazana kupata wale walio bora.
Kuwa na watu wachache bora wanaokukubali kuna manufaa kuliko kuwa na wengi wasio bora.
Kuwa na marafiki wachache ambao ni bora utanufaika kuliko kuwa na wengi ambao siyo bora.
Na kuwa na wateja wachache ambao ni bora, utawahudumia vizuri, wataridhika na utaweza kupiga hatua kubwa.

Dunia inatuhadaa na wingi, lakini wingi huo umekuwa hauna msaada.
Chenye msaada kwako ni ubora, hivyo kwenye kila eneo la maisha yako kazana upate watu ambao ni bora kabisa.

Na haimaanishi ulichagua kuwa na watu bora basi lazima uwe nao wachache.
Utaanza na wachache, lakini baadaye watakua wengi, ila wote watakuwa bora kama utasimamia kupata walio bora.

Pia usisumbuke sana na wale wasiokukubali,
Bali angalia kwanza ubora wao.
Utagundua wengi hawana ubora wa viwango ulivyojiwekea,
Hivyo hawapaswi kukufanya hata ujali,
Maana hao siyo unaowataka.

Mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii inatusukuma kuangalia wingi na siyo ubora,
Wingi wa marafiki, wingi wa wafuasi, wakati watu hao hata hawakujui vizuri.
Ya nini kusumbuka na watu ambao unaweza kupishana nao barabarani na wasikujue?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuanza na kikundi kidogo, fungua hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/11/2050

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
http://www.mafanikio.substack.com