“Two ways exist to guide human activity. One is to force a person to act against his wishes; the other is to guide a person’s wishes, to persuade him with reasoning. One is the used by ignorant people, and it leads complete disappointment. The other is supported by experience, and is always successful.” — Abraham Comb
Kuna njia mbili za kuwabadili watu,
Njia ya kwanza ni kuwashurutisha au kuwalazimisha kufanya kinyume na matakwa yao.
Njia hii huwa inahitaji nguvu kubwa, lakini matokeo yake huwa siyo mazuri.
Kwa sababu mtu akishajua analazimishwa kitu, basi atafanya kinyume na anavyolazimishwa.
Njia ya pili ni kuwashawishi watu kupitia matakwa yao na kuwafanya wachague wenyewe kufanya kitu kwa sababu kinawapa manufaa.
Njia hii haihitaji nguvu kubwa, ila inahitaji muda.
Njia hii ina matokeo mazuri na ya uhakika.
Njia ya shuruti imekuwa inatumiwa na wajinga wasiokuwa na uelewa wa saikolojia ya mwanadamu.
Wale ambao wamepata nafasi au mamlaka fulani na kufikiri mamlaka hayo yanawapa nguvu za miujiza.
Njia ya ushawishi imekuwa inafanya vizuri na matokeo yake kudumu muda mrefu, kwa sababu mtu anakuwa amechagua mwenyewe.
Mifano iko wazi,
Kwa upande wa serikali, serikali zote za kidikteta zilizowahi kutokea duniani, zilifanya maendeleo makubwa, lakini hazikuishia pazuri.
Ni kwa sababu watu walikuwa wanafanya kwa kushurutishwa.
Kwa upande wa mfumo wa uchumi, ujamaa ulishindwa vibaya kwa sababu unatumia shuruti, ni lazima ufanye na uwe kama wengine.
Ubepari umeweza kuendelea licha ya mapungufu yake kwa sababu unatumia ushawishi na siyo nguvu.
Upo usemi kwamba unaweza kumlazimisha farasi kwenda mtoni, lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.
Wanaoshindwa kufanya hivyo ni wale wanaotumia nguvu.
Lakini ukitumia ushawishi, ni rahisi kumfanya farasi anywe maji.
Unajua kabisa kwamba kiumbe yeyote akiwa na kiu lazima atafute na kunywa maji.
Hivyo kabla hujampeleka farasi huyo mtoni, mpe kwanza pumba yenye chumvi.
Halafu mfikishe mtoni na muache tu, mwenyewe atayakimbilia maji.
Hiyo ndiyo nguvu ya ushawishi.
Mara zote tumia ushawishi na siyo shuruti.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kuwafanyia wengine kwa ajili yako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/13/2052
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.