“Winning is great, sure, but if you are really going to do something in life, the secret is learning how to lose. Nobody goes undefeated all the time. If you can pick up after a crushing defeat, and go on to win again, you are going to be a champion someday.” – Wilma Rudolph
Kila mtu anataka mafanikio kwenye maisha, kila mtu anataka ushindi.
Lakini kuna kitu kimoja tunachokijua, hakuna anayeshinda mara zote.
Hata kwenye michezo, timu inayopata ushindi wa jumla na kuchukua kombe, siyo kwamba inakuwa imeshinda michezo yake yote, kuna ambayo ilipoteza.
Tatizo la ushindi ni kwamba huwa hatujifunzi.
Ni vigumu sana kujifunza ukiwa umeshinda,
Kwa sababu ushindi unakupa kiburi, unakufanya uone tayari unajua na kuweza kila kitu.
Ushindi pia unakupa upofu, unakuzuia kuona mchango wa vitu vingine kama bahati kwenye nafanikio yako.
Hii ndiyo sababu mara nyingi kinachofuata baada ya ushindi ni anguko.
Kushindwa, japo kunaumiza lakini kuna faida moja kubwa, kunatupa unyenyekevu na utayari wa kujifunza.
Kushindwa kunatufanya tuone wazi kipi ambacho hatukijui na wapi ambapo tunakosea.
Tunaposhindwa, tunakazana kujifunza ili tusishindwe tena.
Kwa namna hiyo, kushindwa kunakuwa na manufaa makubwa kwetu, kunatusukuma kupata ushindi wakati mwingine.
Ushindi ni mzuri, lakini kama unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, jifunze kupitia kushindwa kwako.
Kwa sababu hakuna anayeweza kushinda kila wakati, usikubali kushindwa kuwe kikwazo kwako.
Kama utaweza kuamka tena baada ya kuanguka,
Na kwenye kupambana kwa ubora zaidi,
Siku moja utafika kwenye ushindi mkubwa.
Muhimu kabisa ni kujijengea tabia ya kufanya tathmini kwa kila matokeo unayopata, iwe ni ushindi au kushindwa.
Angalia kipi umefanya vizuri, kipi umekosea na upi mchango wa bahati nzuri au mbaya.
Kisha panga hatua bora zaidi za kuchukua wakati mwingine.
Ukijijengea nidhamu hii, utafanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kupanga hatima ya maisha yako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/14/2053
Pia kama hujasoma mjadala wa kwenye Mwongozo Wa Mafanikio kuhusu nguvu ya msimamo, soma hapa na uweke maonj yako; http://www.mafanikio.substack.com/p/sahihi-kumi-na-tatu-tu-nguvu-ya-msimamo
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante Sana kocha kwa tafakari hii, mafanikio sio lelemama ni mapambano, ukiona mtu au kampuni imesimama vizuri haimanishi kuwa huko nyuma haikuwa na changamoto,kuanguka isiwe Sababu ya kutokusimama tena, Kama unazijua namba zako ni kuzipigania ili uzifikie.asante sana mental wangu.
LikeLike
Ni kweli kabisa Beatus.
LikeLike