“Tell me to what you pay attention, and I’ll tell you who you are.” – Ortega y Gasset
Kile unachokipa umakini wako, ndiyo kinachokutengeneza.
Hivyo ukitaka kujua utakuwa mtu wa aina gani,
Angalia vitabu unavyosoma sasa,
Angalia habari na mitandao unayofuatilia,
Na angalia wale unaotumia nao muda wako mwingi.
Sisi binadamu ni rahisi sana kushawishika na wengine.
Unaweza kuwa na wazo bora la kufanya kitu, ukiamini litakuwezesha kufanikiwa.
Unakuwa na shauku kuhusu wazo hilo na kwenda kuwaambia watu wako wa karibu.
Na wao wanaanza kukuonesha kwa nini wazo hilo halifai au haliwezi kufanya kazi.
Unaweza kulitetea lakini utakapotoka hapo utatafakari tena na kuona watu hao walikuwa sahihi.
Hutaweza kujiamini tena kama mwanzo na wazo hilo litakuwa limeishia hapo.
Fikra zinazotawala akili yako kwa muda mrefu, ndizo zinazokutengeneza wewe.
Hivyo kama unataka kuyabadili kabisa maisha yako, anza na fikra zako.
Badili kabisa yale unayofikiri na kuyapa umakini wako.
Badili aina ya vitabu unavyosoma,
Achana na habari, mitandao na watu hasi.
Linda sana akili yako, usiruhusu ichafuliwe na chochote.
Maana hiyo ndiyo inayajenga maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa kwa kusoma leo ni kuhusu kulinda uhuru wako wa mbeleni, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/17/2056
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.