Don’t be afraid of a person in any position, in low or high standing, whether he is a scholar or an ignorant person. If you respect all people, you should love all people, and fear no one. —William Ellery Channing

Hupaswi kumwogopa mtu yeyote kwenye maisha yako.
Bali unapaswa kumheshimu kila mtu, unapaswa kumpenda kila mtu.
Tunawajua wengi ambao wamezikosa fursa nzuri kwenye maisha yao kwa kuwadharau watu kwa mwonekano wa nje, baadaye wakaja kugundua watu hao ni muhimu sana.
Tunawajua wengi ambao wanaishi maisha yao kwa hofu na kushindwa kusimamia ukweli kwa sababu wanawaogopa wale wenye nafasi kubwa kuliko wao, iwe ni bosi, kiongozi au ndugu.

Usiogope, bali heshimu.
Kuogopa kunakufanya uwe mtumwa, kunakunyima uhuru na kukufanya ujione hustahili.
Lakini kuheshimu na kupenda kunakuweka huru, kunakufanya uthaminike na wengine.

Unayemwogopa, ana kudharau na kuona anaweza kukutumia atakavyo.
Unayemheshimu anakuheshimu pia na atajua mipaka iko wapi.

Watu wengi unaokutana nao kwenye maisha yako ya kila siku huwajui,
Hujui nafasi zao wala mchango wanaoweza kuwa nao kwenye maisha yako ya baadaye.
Ukijiwekea msimamo wa kumheshimu kila mtu, hutakosea wala kuharibu mahusiano yako na wengine, iwe unawajua au huwajui.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu umuhimu, usahihi na ufanisi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/22/2061
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.