“In order to hit the mark, you should aim farther than it stands, so you will achieve it; in order to be just, you should make a self-sacrifice, be unjust to yourself.” – Leo Tolstoy
Ili kufikia lengo, unapaswa kulenga mbali zaidi ya lengo hilo.
Ukilenga kwa kiasi hicho hicho unachotaka, unaishia kupata chini yake.
Hivyo lenga mbali zaidi, ili unapopata pungufu uangukie kwenye lengo lako la awali.
Na kiwango cha ziada unachopaswa kulenga ni mara 10 zaidi.
Lenga kupata mara kumi ya kile unachotaka,
Hapo utajisukuna zaidi.
Na hata kama hutapata mara kumi, lazima utafikia lengo lako la awali.
Huwa tunakosea kwenye mipango na makadirio tunayojiwekea, ndiyo maana mipango mingi tunayojiwekes hatuifikii.
Ni kwa sababu hatuweki nafasi zaidi, tunapanga kwa kiwango kile kile tunachotaka.
Ondokana na hilo kwa kupanga kwenda mbali zaidi na utafika kwenye lengo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ukweli ni sasa, kama unataka kuishi maisha ya kweli, ishi sasa, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/25/2064
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.