“Freedom is not something that anybody can be given; freedom is something people take and people are as free as they want to be.” – James Baldwin

Chochote kile unachosubiria watu wengine wakupe, unapoteza muda wako.
Hiyo ni kwa sababu hakuna yeyote mwenye nguvu ya kukupa chochote unachotaka, bali wewe mwenyewe.
Kama unataka kuwa huru kwenye maisha yako, usisubiri wengine wakupe uhuru, bali chukua uhuru wako mwenyewe.
Kama unataka kuwa na furaha, kusubiri wengine wakupe ni njia mbovu ya kuipata, unachopaswa ni kujipa wewe mwenyewe.

Wewe ndiye mwenye mamlaka ya kwanza kwenye maisha yako, hakuna mwingine mwenye mamlaka juu yako.
Kwa maana hiyo basi, jukumu kubwa la maisha yako ni lako mwenyewe,
Usisubiri mwingine ndiye achukue hatua,
Usilaumu wala kumlalamikia mwingine yeyote.
Shika hatamu ya maisha yako na piga hatua unazotaka kupiga.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu dawa ya hasira, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/29/2068

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.