“You don’t have to turn this into something. It doesn’t have to upset you. Things can’t shape our decisions by themselves.” – Marcus Aurelius

Matukio huwa yanatokea kama yalivyopanga yenyewe,
Na yanatokea kwa kila mtu.
Ila baadhi ya watu wamekuwa wanayabadili matukio hayo na kuwa mzigo zaidi kwao.
Usiingie kwenye kundi hilo.
Badala yake chukulia kila tukio kama linavyotokea,
Usianze kulipa maana yako,
Kwa kufanya hivyo unajijaza hofu, kujiumiza na kujikatisha tamaa.

Kwa kila kinachotokea kwako, chukulia kama kinatokea kwa mtu mwingine.
Yale yanayotokea kwa wengine huwa tunaona ni kawaida, tunaweza hata kuwapa moyo na kuwashauri wasijali, mambo yatakuwa vizuri.

Lakini kitu hicho hicho kikitokea kwako unaona kama ni mwisho wa dunia.
Unajijaza hofu na kukata tamaa.
Siyo kwamba yanayotokea kwako ni makubwa kuliko yanayotokea kwa wengine,
Bali unayaona makubwa kwa sababu ndiyo unayatafsiri hivyo.
Chagua sasa kuyaona matukio kama yalivyo na utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuyatatua.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu gharama ya umaarufu, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/08/30/2069

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.