“Do not bother about what will happen someday, some where, in the far away distance, in a future time; think and be very attentive to what happens now, here, in this place.” — John-Ruskin
Wasiwasi, hofu na mashaka ni matokeo ya mtu kusumbuka na mambo ambayo bado muda wake haujafika.
Ni sawa na kufikiria daraja ambalo hujalifikia,
Unaweza kuhofia utakavyo, lakini hutalivuka mpaka utakapolifikia.
Ya nini sasa kusumbuka na daraja ambalo bado hujalifikia?
Kwa nini usiendelee na safari yako mpaka kulifikia daraja?
Kwenye maisha, wengi wanaishia njiani kwa kuhofia mambo ambayo bado hawajayafikia.
Wakiangalia ukubwa wa kule wanakokwenda, wanaona hakuna namna watafika, hivyo wanaacha
Iwapo mtu angeacha kuhofia ukubwa wa mbele na kuangalia kile anachoweza kufanya sasa, hatua kwa hatua atajikuta amefika mbali.
Usiruhusu ambayo hujayafikia yawe kikwazo kwako.
Mara zote angalia kilicho mbele yako sasa, na chukua hatua za kukifanya kwa ubora.
Hilo ndilo unalohitaji ili kufanikiwa,
Kukabiliana na kila lililo mbele yako kwa wakati huo na kutokuogopa ambalo hujalifikia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu magumu matatu ya kiroho, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/05/2075
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani
Asante sana kocha kwa somo la kushinda hofu.
LikeLike