“People hasten to judge in order not to be judged themselves. What do you expect? The idea that comes most naturally to man, as if from his very nature, is the idea of his innocence.” ~ Albert Camus

Wanaokimbilia kuhukumu ni wale ambao hawataki kuhukumiwa.
Wanajijua kabisa kwamba wana hatia na hivyo wanachukua hatua ya kuwahukumu wengine haraka ili watu wasipate nafasi ya kuwaangalia wao na kuona hatia zao.

Wanaokimbilia kukatisha wengine tamaa ni wale ambao wameshakata tamaa na maisha yao. Watu hao hawapo tayari kuona wengine wakiwa na matumaini wakati wao hawana.

Wanaokimbilia kukosoa wengine ni wale ambao hawapo tayari kufanya.
Kufanya jambo lolote ni kugumu sana, kukosoa ni rahisi.
Wale ambao hawawezi kufanya, hutafuta sifa kwenye kukosoa.

Matendo ya kila mtu kuna kitu yanaficha,
Hivyo kabla ya kuamini kile ambacho mtu anakiigiza kwako, angalia kwanza ni nini anachoficha.
Ukishajua anachoficha mtu, utaweza kujua ni uzito kiasi gani unapaswa kuweka kwenye kile anachosema.

Usiumizwe na yale wanayosema au kufanya wengine,
Bali kazana kufanya kile ulichochagua kufanya,
Ukikifanya kwa ubora na kuendelea kujifunza kadiri unavyokwenda.
Na usiwapangie wengine jinsi ya kukuchukulia wewe,
Watakuchukulia kwa namna waliyochagua wenyewe, kutokana na kile wanachoficha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#NidhamuUadilifuKujituma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu hadithi za mafanikio ya wengine zinavyoweza kuwa kikwazo kwako, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/09/2079

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.