“A wise man looks for everything inside of himself; a mad man seeks for everything in others.” —Confucius

Mwenye hekima hutafuta kila kitu ndani yake,
Mpumbavu hutafuta kila kitu nje yake.
Mwenye hekima anajua maisha yake ni jukumu lake na analibeba kila ya kulalamika au kunung’unika.
Mpumbavu anaona maisha yake ni jukumu la wengine na kila wakati ana watu wa kulaumu au kulalamikia.

Mwenye hekima anaposhindwa au kukwama, anaangalia ndani yake nini kinakosekana.
Mpumbavu anaposhindwa au kukwana anatafuta nje nani kasababisha.
Kwa tofauti hizi mwenye hekima anapiga hatua na kufanikiwa,
Huku mpumbavu akibaki pale alipo au kurudi nyuma zaidi.

Ukitaka kujipima iwapo utapiga hatua au utarudi nyuma, anza kwa kuangalia unatafuta vitu ndani yako au nje yako.
Kama umekuwa unatafuta nje, ni wakati wa kubadilika sasa na uanze kutafuta ndani yako.
Majibu sahihi, hatua bora za kuchukua, vyote viko ndani yako.
Bila kujiuliza na kujisikiliza, huwezi kuyapata majibu hayo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mambo matatu yatakayokujengea heshima, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/10/2080

Rafik yako,
Kocha Dr Makirita Amani.