“Tell me to what you pay attention, and I’ll tell you who you are.” – Ortega Gasset
Mtu yeyote, asiyejua chochote kuhusu wewe, anaweza kutabiri kwa usahihi wewe ni mtu wa aina gani, kwa kuangalia vitu unavyojisumbua navyo.
Kule unakopeleka umakini wako na nguvu zako, ndiko kunakukujenga.
Unakuwa kile unachofikiri na kufanya muda wako mwingi.
Unachofikiri kinachochewa na yale unayojifunza na kufuatilia.
Ukitaka kujua utafika wapi na maisha yako, angalia wale wanaokuzunguka wamefika wapi.
Maana hao wana nguvu kubwa ya kukutengeneza wewe kuliko wewe mwenyewe.
Kama unataka kuwa na maisha unayoyataka wewe,
Kwanza dhibiti umakini wako kwa kuchagua kuhangaika na mambo yenye tija kwako tu.
Pili peleka nguvu zako na muda wako kwenye yale muhimu kwako, yanayokufikisha unakotaka kufika.
Tatu angalia wale wanaokuzunguka na hakikisha unazungukwa na watu waliopiga hatua au wanaokazana kupiga hatua. Epuka kuzungukwa na waliokata tamaa.
Ishi kila siku kwa kudhibiti umakini, nguvu na muda wako,
Maana hizo ni rasilimali zinazkwindwa na wengine,
Usipopambana nazo kuzilinda, wengine watazitumia kwa manufaa yao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kanuni ya maisha rahisi kutoka kwa Epictetus, isome hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/11/2081
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Nakushkru sana kocha kwa tafakari hii, Elimu hii inayabadilisha maisha yangu,sina hofu,sina woga,silalamiki wala kulau wengine,sio sasa mtu wa kukata tamaa, hakika nakushkru sana kocha wangu na Ubarikiwe Sana.
LikeLike
Vizuri Beatus kwa hatua kubwa unazopiga kwenye maisha yako,
Endelea kujifunza na kuwa bora zaidi.
Kila la kheri.
LikeLike