“A wise man has doubts even in his best moments. Real truth is always accompanied by hesitations. If I could not hesitate, I could not believe.” — Henry David Thoreau
Mara zote ukweli huwa ni mgumu,
Na huwa unaambatana na wasiwasi,
Kwa sababu wengi huwa hawakubaliani nao.
Ni hali hii ndiyo inawafanya wengi kutokupenda ukweli,
Badala yake kuamini kile ambacho wengine wanaamini.
Uongo huwa unaaminika kirahisi, ndiyo maana wengi huangukia kwenye uongo.
Uongo huwa hauna wasiwasi, kwa sababu umetengenezwa makusudi kujibu kila wasiwasi ulipo.
Usiukimbie ukweli kwa sababu hauna uhakika nao kwa asilimia 100.
Usitake ukweli uondokane na kila aina ya wasiwasi.
Kuwa tayari kuukabili ukweli na wasiwasi wake,
Na hapo utakuwa kwenye njia rahisi.
Ogopa sana wale wanaoyafanya mambo magumu kuonekana rahisi,
Ogopa wale wanaokuambia unapaswa kuamini bila kuhoji,
Usikubaliane na wale wanaokuondoa kwenye ukweli kwa sababu kuna wasiwasi,
Ukweli siyo rahisi,
Ukweli huwa haubembezi,
Na ukweli huwa haufichwi daima.
Usiukimbie ukweli na kwenda kuamini vitu vya uongo.
Mara zote simama kwenye ukweli, hata kama huna majibu ya kila kitu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kukuza hofu au kuchukua hatua, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/14/2084
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.