Rafiki yangu mpendwa,

Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa kihistoria, umekuwa mwaka ambao ni mrefu na mfupi kwa wakati mmoja.

Umekuwa mwaka mrefu kwa matukio mengi ambayo yametokea na kutikisa dunia kwa muda mfupi.

Lakini pia umekuwa mwaka mfupi kwa sababu unaonekana kuisha haraka.

Wakati tunauanza mwaka kila mtu alikuwa na malengo makubwa, hakuna aliyeona kinachokuja mbele.

Haikupita miezi mingi dunia nzima ikasimama na mambo mengi yakasimama na hali hiyo ikamgusa kila mtu, bila ya kujali anajihusisha na nini.

Ni kwa matukio hayo watu wamekuwa na utani mbalimbali kuhusu mwaka 2020.

Wapo wanaosema mwaka ufutwe na tuanze upya, wengine wanasema ni mwaka ambao tumeishi muongo mzima ndani ya mwaka mmoja.

Mimi nina kitu kimoja cha kukuambia, mwaka 2020 umetuonesha kipi muhimu kwenye maisha yetu na kipi ambacho siyo muhimu.

Tunapokwenda kuumaliza mwaka 2020 na kuuanza mwaka 2021 ambao una fursa ya kuwa mwaka bora kuwahi kutokea, nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya mafunzo na ukocha ambayo nimekuwa naiendesha kwa miaka sita sasa. Programu hii ina watu wenye kiu kubwa ya kufanikiwa kutoka kila mkoa wa nchi ya Tanzania, na wengine kutoka nchi jirani.

Kwa kuwa wanachama wametawanyika nchi nzima, kila mwaka huwa tunakutana mara moja kwenye mkutano mkubwa wa wanamafanikio wote.

Tumekuwa tunafanya mikutano hii kwa miaka minne sasa, tangu mwaka 2016 bila kuacha.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018

Na mwaka huu 2020, pamoja na yote ambayo yametokea, tunapata tena nafasi ya kukutana pamoja kwenye mkutano huu mkubwa wa kimafanikio ili tuweze kupeana mikakati ya kupiga hatua zaidi na kufikia mafanikio makubwa.

Ninayo furaha kukujulisha kwamba SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 itafanyika jumapili ya tarehe 15/11/2020 jijini Dar es salaam.

Kwenye semina hii, tunakwenda kujifunza na kupata hamasa ambayo itatuwezesha kufanya makubwa zaidi kwa mwaka unaokuja mbele yetu.

Yafuatayo ni baadhi ya mengi utakayojifunza kwenye semina ya mwaka huu 2020;

1. JINSI YA KUONDOKA KWENYE HALI YA UCHOVU NA KUKOSA HAMASA (BURNOUT)

Kwa yale yaliyotokea mwaka huu 2020, kila mtu amechoka kupitiliza, hamasa kwa wengi imeshuka mno. Ule msukumo wa kufanya makubwa umepungua na kupotea kabisa kwa wengi.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 tunakwenda kujifunza jinsi ya kuondoka kwenye hali ya uchovu na kukosa hamasa, inayojulikana kwa Kiingereza kama burnout. Utajifunza mbinu ambazo zitakuwezesha kuendelea kujisukuma bila ya kujali nini kinaendelea kwenye maisha yako au duniani.

2. MPANGO WA MUONGO WA 2020 – 2030

Watu wamekuwa wanadanganywa kuna njia ya mkato ya kufanikiwa, wanajaribu kila njia na kujikuta wamerudi pale pale. Wengine wamekuwa wanakimbizana na kila fursa inayojitokeza mbele yao, lakini mwisho wa siku wanajikuta hawajapiga hatua yoyote.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 utajifunza jinsi ya kuweka mpango utakaoufanyia kazi kwa muongo (miaka kumi) mzima wa 2020 – 2030. Utatoka kwenye semina ukiwa umeshaamua unakwenda kupambana na nini na kuachana na usumbufu mwingine wowote.

3. LENGO KUU LA MWAKA WA MAFANIKIO 2020/2021

Wakati watu wa kawaida wakianza mwaka mpya tarehe moja ya mwezi wa kwanza kwenye mwaka husika, sisi wanamafanikio huwa tunauanza mwaka mapema kabisa, wiki nane kabla ya watu wa kawaida.

Mwaka wetu wa mafanikio huwa unaanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba na kumalizika wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba mwaka unaofuata. Kwa kuanza mwaka wa mafanikio mapema, tunakuwa mbele zaidi na hatuanguki kwenye mkumbo wa wale wanaoweka malengo kwenye mwaka mpya kwa sababu kila mtu anaweka malengo.

Semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 itakuwa ni ufunguzi wa mwaka wetu wa mafanikio 2020/2021 hivyo pia utapata nafasi ya kuweka na kushirikisha malengo yako ya kimafanikio kwa mwaka huo wa mafanikio. Usikose semina hii ili uweze kuuanza mwaka 2021 mapema kabisa, mpaka wengine wanapokuja kuamka, wewe umeshafanya makubwa.

4. MWONGOZO WA MWAKA WA MAFANIKIO 2020/2021

Kila mwaka wa mafanikio huwa tuna kitu kinatuongoza kwa mwaka mzima. Kitu hicho ndiyo kinapima kila kipaumbele na mengine yote yasiyoingia kwenye mwongozo huo yanakaa pembeni.

Mwaka huu wa mafanikio 2019/2020 tunaoumaliza mwongozo ulikuwa KIPATO ZAIDI 2020, ambapo mpango ni kuongeza kipato kwa asilimia 20. Kwa mwaka mzima tumefanyia kazi mwongozo huo na watu wameweza kufanya makubwa, licha ya changamoto zilizoukumba mwaka huu.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 utakwenda kujifunza na kuondoka na mwongozo wa kufanyia kazi mwaka 2020/2021 ambao utakuwezesha kufanya makubwa kwenye mwaka huo.

5. SHUHUDA ZA WANAMAFANIKIO

Sehemu nzuri kabisa ya mkutano wa KISIMA CHA MAARIFA ni shuhuda zinazotolewa na wanamafanikio mbalimbali. Unajionea wazi jinsi ambavyo watu wanapiga hatua na kufanya makubwa, bila ya kukubali sababu zozote kuwarudisha nyuma.

Unapotoka kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA unakuwa na nguvu, msukumo na hamasa kubwa ya kwenda kufanya makubwa pia.

Kwenye semina ya mwaka huu 2020 kuna shuhuda kubwa na nzuri kutoka kwa wanamafanikio ambao wameweza kupambana licha ya ugumu tuliopitia na hizo zitakuondolea kila sababu unayojipa kama kikwazo cha mafanikio yako.

6. KUWEKA MIKAKATI NA NJIA ZA KUJIFUATILIA 2020/2021

Kuweka malengo ni rahisi, kupanga mipango ni rahisi pia, lakini inapokuja kwenye utekelezaji, hapo ndipo wengi wanapokwama.

Wengi wamekuwa wanalalamika kwamba wakihudhuria mikutano au semina mbalimbali wanatoka wakiwa na hamasa, lakini siku chache baadaye hamasa ile inakuwa imepoa na wanarudi kwenye mazoea yao.

Semina za KISIMA CHA MAARIFA ni tofauti kabisa, kwani hizi zina njia ya kukupa hamasa kwa mwaka mzima tangu uliposhiriki semina. Kwenye semina hizi huwa natoa nafasi chache na adimu za programu ya ukocha ambapo nakufuatilia kwa karibu kutekeleza yale uliyojipangia. Na unapokuwa kwenye programu hizo, sikuachii kirahisi.

Karibu ushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 na upate nafasi ya kuwa na hamasa ya kufanya makubwa kwa mwaka mzima, kwa kuwa chini ya ufuatiliaji wa karibu wa kocha.

7. UZINDUZI WA VITABU VIWILI; NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kila mwaka kwenye semina hizi huwa nazidua vitabu vipya vya mafanikio, mwaka jana ilikuwa kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 nitakwenda kuzindua vitabu viwili muhimu mno kwenye zama tunazoishi na yale yanayokuja mbele yetu. Vitabu hivyo ni UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA na ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA. Watu wamekuwa hawajui nguvu kubwa iliyo ndani yao ya kuwawezesha kufanya makubwa, kitabu hicho kitakuonesha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa. Pia kitabu cha elimu ya msingi ya biashara kinakupa mafunzo muhimu ya kuanzisha na kukuza biashara yako. Usikose semina hii, kwani ndiyo sehemu pekee utakapoweza kupata nakala zilizosainiwa za vitabu hivyo.

8. NA MENGINE MENGI.

Watu mnapokutana, kuna mengi sana ambayo huwa yanatokea, mengi huwezi kuyaelezea. Kila mwaka ninapoandaa semina hizi, hutokea watu wapya ambao hawajawahi kushiriki na wapo njia panda, iwapo washiriki au la. Mimi huwa nawaambia washiriki kama jaribio, na kama semina haitakuwa na manufaa kwao, basi wanaweza kudai gharama walizolipa.

Mtu mmoja niliyewahi kumwambia hivyo, siku ya semina, kabla hata haijaisha alinifuata na kuniambia kwa nini usiwe unaandaa semina hizi mara mbili kwa mwaka? Aliona thamani kubwa ambayo hakutegemea, na ilimsaidia sana.

Usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 ambapo tunakwenda kujifunza mengi na kuondoka na nguvu na hamasa ya kufanya makubwa 2020/2021.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

UTARATIBU WA SEMINA.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dar es salaam, kwenye moja ya hotel, taarifa zaidi utazipata baada ya kuamua kushiriki.

LINI; Jumapili ya tarehe 15 mwezi Novemba 2020, semina ni ya siku nzima, kuanzia saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku.

ADA; Gharama za kushiriki semina hii ni tsh 200,000 (laki mbili) ambayo itagharamia kila kitu kwa siku ya semina pamoja na kuwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima ukipata mafunzo kila siku.

KUSHIRIKI; Ili kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2020 unapaswa kutoa taarifa mapema (leo hii) kwa kutuma ujumbe wenye majina yako kamili na namna ya simu na kueleza NITASHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020. Ujumbe unautuma kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

MALIPO; Malipo ya ada ya kushiriki semina yanafanywa kwa njia ya MPESA 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money kwenda namba 0717 396 253 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma malipo, tuma ujumbe ukieleza umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020. Unaweza kufanya malipo kidogo kidogo.

MWISHO WA MALIPO; Tarehe ya mwisho kufanya malipo ni 10/11/2020.

Karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, karibu tupate nafasi ya kuuanza pamoja mwaka mpya wa mafanikio, tutoke tukiwa na nguvu na hamasa ya kwenda kufanya makubwa ili tufanikiwe zaidi.

Chukua hatua sasa ili ujihakikishie nafasi ya kushiriki semina hii, tuma ujumbe wa kushiriki kwa wasap namba 0717396253.

Naamini tutakuwa pamoja kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020, karibu sana.

Rafiki yako,

Kocha Dr Makirita Amani.