“If a man is to achieve all that is asked of him, he must take himself for more than he is, and as long as he does not carry it to an absurd length, we willingly put up with it.” – Johann Wolfgang von Goethe

Ni hesabu rahisi kabisa kwamba kupata matokeo ya tofauti na unavyopata sasa, lazima ufanye tofauti na unavyofanya.
Ili upate zaidi lazima ufanye zaidi.

Lakini cha kushangaza, wengi wanataka wapate matokeo tofauti, huku wakiendelea kufanya walichozoea kufanya.

Kwenye mafanikio, inashangaza jinsi wengi wanavyoyatamani mafanikio, wanavyosoma hadithi za waliofanikiwa, wanavyoweka mipango ya mafanikio,
Lakini hawataki kubadilika, wanataka waendelee kuwa kama walivyo sasa, lakini wayapate mafanikio wanayotaka.
Hicho ni kitu kisichowezekana kabisa.

Kila unapofikiria kupata matokeo ya tofauti na unayopata sasa, anza kujiuliza ni kwa namna gani unapaswa kuwa tofauti na ulivyo sasa.
Kama haitaanzia ndani yako na ukabadilika wewe,
Hakuna cha nje kitakachobadilika.

Badili mtazamo ulionao,
Badili fikra ulizonazo,
Badili hatua unazochukua,
Na hapo matokeo unayopata yatakuwa tofauti.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu gharama ya kusimamia ukweli, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/15/2085

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.