“There are no accidents so unfortunate from which skilful men will not draw some advantage, nor so fortunate that foolish men will not turn them to their hurt.” – François Duc De La Rochefoucauld

Huyachukulii mambo kwa jinsi yalivyotokea,
Bali unayachukulia mambo jinsi ulivyo wewe.
Hata kama kumetokea jambo baya kiasi gani, mwenye hekima huwa hakosi cha kujifunza na kunufaika na jambo hilo.
Na hata kama kumetokea jambo zuri kiasi gani, mpumbavu huwa hakosi cha kuumizwa na jambo hilo.

Hivyo, wenye hekima hunufaika na kila kinachotokea, hata kama ni kibaya kabisa.
Huku wapumbavu wakiumizwa na kila kinachotokea, hata kile ambacho ni kizuri kabisa.

Badala ya kusumbuka na yale yanayotokea, anza kusumbuka na wewe mwenyewe.
Ili kuwa na maisha bora na tulivu, huhitaji kudhibiti yale yanayotokea, hilo liko nje ya uwezo wako, bali unapaswa kujidhibiti mwenyewe, ambalo liko ndani ya uwezo wako.

Ukiweza kunufaika na kila unachokutana nacho, hata kama ni kibaya kiasi gani, utakuwa umepiga hatua kubwa kiutambuzi binafsi na kujidhibiti mwenyewe.
Kwa zama tunazoishi sasa, upumbavu na hekima ni hali za kuchagua maana kuna kila fursa ya kujifunza na kuchukua hatua ili kuwa bora zaidi.

Kuwa mwenye hekima, kuwa na udhibiti wa ndani yako na hakuna cha nje kitakachokusumbua.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kinachokupa nafasi ya kujangaika na mambo madogo madogo, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/17/2087
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.