“Most people act, not according to their meditations, and not according to their feelings, but as if hypnotized, based on some senseless repetition of patterns.” – Leo Tolstoy
Hebu jipe nafasi ya kutafakari kila kitu unachofanya kwenye maisha yako na kujiuliza kwa nini umefanya ulichofanya na kwa namna ulivyofanya?
Je umefanya kwa sababu ndivyo ulivyofikiri na kupanga kufanya?
Au umefanya kwa sababu ndivyo umekuwa unafanya na wengine pia wanafanya?
Ukitafakari hili kwa kina na ukawa mkweli kwako, utashangazwa na majibu utakayoyapata.
Utaona wazi kwamba kinachokusukuma kufanya ni mazoea na mkumbo.
Unafanya leo kwa sababu ndivyo ulivyofanya jana na kesho utafanya kwa sababu leo umefanya.
Pia unafanya kitu kwa sababu wengine wanaokuzunguka nao wanafanya na wanakutegemea na wewe ufanye pia.
Kwa kwenda hivi, huwezi kufanikiwa, hata kama unajituma kiasi gani.
Kwa sababu mafanikio hayaji kwa mazoea au mkumbo, bali yanakuja kwa upekee na utofauti.
Kila mara angalia kile unachofanya na kisha jiulize kama kuna njia bora zaidi ya kufanya.
Kila wakati jaribu namna mpya na bora za kufanya unachotaka kikupeleke kwenye mafanikio makubwa.
Ukiweza kuvuka mazoea na mkumbo, ukiweza kuwa wewe na kufikiri pamoja na kupanga kila unachofanya, utazalisha matokeo ya tofauti na ambayo yatakufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Kuwa wa tofauti na wa kipekee, usiende kwa mazoea wala kufuata mkumbo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mambo yanavyoanza kwa nia njema, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/27/2097
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.