“Be wise and self-controlled, and share in courage and justice … the art by which a human would become good. We must do just that!” —Musonius Rufus
Falsafa ya Ustoa ina misingi mikuu minne.
Misingi hiyo tunaweza kuigawa kwenye pande mbili, upande wa kwanza ni kwetu wenyewe na upande wa pili ni kwenye ushirikiano wetu na wengine.
Kwa upande wetu wenyewe, tunapaswa kuwa na HEKIMA na pia tunapaswa KUJIDHIBITI.
Hekima tunaipata kwa kupata maarifa sahihi na kisha kuyaweka kwenye matendo, kuishi kwa namna iliyo bora zaidi.
Kujidhibiti ni kuwa na kiasi kwenye kila unachofanya.
Kwa upande wa ushirikiano na wengine, tunapaswa kuwa na UJASIRI na pia kuwa na HAKI.
Kwa ujasiri tunafanya kile kilicho sahihi bila kujali gharama au madhara yake, mara zote tunasimama upande sahihi.
Na kwenye haki, tunawatendea wengine kile ambacho tungependa kutendewa na sisi pia. Hatutafuti kujinufaisha zaidi huku tukiwaumiza wengine.
Mwanafalsafa Musonius Rufus anatusaidia kuiweka misingi hii ya Ustoa kwenye sentensi moja; “Kuwa mwenye hekima na jidhibiti mwenyewe na shirikiana na wengine kwa ujasiri na haki. Hiyo ndiyo namna ya kuwa mtu mwema, tunapaswa kuishi hivyo.”
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu tabia kama akiba, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/28/2098
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.