Mpendwa rafiki yangu,

Kabla hujaingia kwenye ndoa, ulikuwa na thamani ya matarajio ambayo ulitegemea kuipata baada ya kuwa naye.
Wengi wanaingia kwenye mahusiano na mtu kwa matarajio ya kupata thamani fulani.
Mwanzoni mwa mahusiano mtu huwa anajituma vizuri ili kuweza kufanikiwa lengo lake.

Lakini sasa, shida inaanza pale ambapo mtu ameingia kwenye mahusiano ya ndoa na mtu halafu kile alichokuwa anatarajia kukipata hakioni. Hii inawafanya watu kukinai mahusiano waliyokuwa nayo kwa sababu kile walichokuwa wanakitarajia watakipata hawajakipata.

Hivyo wanakinai mahusiano waliyokuwa nayo na kutamani kutafuta mahusiano mengine huenda wataweza kufanikiwa kwenye matarajio wanayotaka.

Kwahiyo, anayeingia na gia ya thamani ya matarajio fulani katika ndoa lazima atafeli.
Kwa sababu ukishakuta siyo hutokua na hamasa ya kuendelea.

Kila anayeingia kwenye mahusiano ya ndoa ajiandae kukutana na chochote. Yaani ujiandae kukutana na kile unachotarajia na kile usichotarajia ili usije kujiumiza hapo baadaye maana hakuna mtu utayemkuta amekamilika kwa kila kitu.

Wengi wanaoumia ni wale walioingia kwenye ndoa kwa matarajio ya kupata tu kile wanachotaka na pale wanapokutana na matarajio tofauti wanaanza kuona mahusiano ni machungu.

Lakini iko sababu kubwa moja inayoweza kukusaidia wewe kuendelea na ndoa yako badala ya kuikinai. Na sababu hiyo ni Kwanini umeingia kwenye ndoa na huyo ambaye uko nae leo.

Kwanini ndiyo inatoa msukumo wa mtu kutoka ndani na kuendelea kupambania mahusiano yake kwa gharama yoyote ile.

Angalia wanaoingia kwenye wito wowote ule kama hawana kwanini wameingia kwenye wito huo ni ngumu kuendelea kama wakikutana na magumu.

Kama unaingia kwenye biashara na hujui kwanini umeingia kwenye biashara hutochukua muda wa kudumu kwenye biashara hiyo.

Kila mtu akikumbuka kwanini yake iliyomsukuma kuingia kwenye ndoa hawezi kuikiani ndoa yake.

Unamchoka mwenza wako kwa sababu huna ile kwanini. Unajua Kwanini ndiyo dira ya mahusiano. Kama huna kwanini inayokuongoza kwenye mahusiano yako ni rahisi kupotea.

Ukiacha hisia zikuongoze ni rahisi kutekwa lakini ukiwa na kwanini utakua makini.

Kuwa na dira inayokuongoza kwenye mahusiano yako. Hutoweza kuimaliza dunia kwa kutaka kuwa na mahusiano na kila mtu. Lakini unaweza kuimaliza dunia kwa kumpenda mtu mmoja kwa moyo wako wote na kuacha mengine.

Hatua ya kuchukua leo; Jua kwanini iliyokusukuma uingie kwenye mahusiano ya ndoa ambayo unayo leo.

Ingia katika mahusiano ya ndoa ukiwa na matarajio tofauti ya kupata au kutokupata thamani ya matarajio uliyokuwa unataka.

Hivyo basi, ipende ndoa yako kwa moyo wako wote. Angalia sababu kubwa iliyokuvuta kwenye ndoa na kamwe hutokinanai ndoa yako.

Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali.

Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa
http://kessydeo.home.blog ,vitabu nakwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI. Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,
Mwl, Deogratius kessy
0717101505//0767101504
deokessy.dk@gmail.com //
Asante sana