“I had spent my whole life trying to fit in, but it would take the rest of my life to realize that some men are just meant to stand out.” — Charles M. Blow

Dunia imakuwa inakuhadaa,
Kwa maisha yako yote umekuwa unashawishiwa kwamba unapaswa kufanana na wengine,
Kwamba unapaswa kuishi na kufanya kama wengine wanavyofanya.
Na kama unatofautiana na wengine, basi dunia imekushawishi uamini kwamba una matatizo.

Umeisikiliza dunia,
Umehangaika sana kufanana na wengine,
Lakini hilo limekufikisha wapi?
Limekufanya uyapende maisha yako?
Limekufanya upate kile unachotaka?

Majibu ni hapana,
Pamoja na kukazana kuwa kama wengine, umeishia kuwa na maisha usiyoridhika nayo.
Hata kwa nje unapoonekana uko vizuri, ndani yako unaujua ukweli, kwamba kuna shimo ambalo halijaweza kujazwa kwa aina hiyo ya maisha.

Unachopaswa kujua ni kwamba watu wote tunatofautiana,
Na ili uweze kuwa na maisha ya mafanikio na unayoyafurahia, unapaswa kuishi kama wewe na siyo kuishi kama wengine.
Unapaswa kufanya yale yenye maana kwako na siyo yanayofanywa na wengine.
Unapoyaishi maisha yako kama wewe, unaridhika nayo na haijalishi wengine kwa nje wanayaonaje, ndani yako unakuwa na utulivu mkubwa.

Maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa kujilazimisha kuwa kama wengine, badala yake kuwa wewe.
Kwa kuwa wewe, hakuna anayeweza kushindana na wewe, hivyo utapata kilicho bora kwako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu watu kusambaza kile walichonacho, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/04/2104

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.