“Define what success means to you in controllable metrics, then edit your life of anything which is going to distract you from that.” – Ben Bergeron
Hivi ndivyo watu wengi wanavyoyapoteza maisha yao,
Wanafanya kile ambacho wengine wanafanya,
Lakini wanapopata matokeo ambayo wengine wanapata, hawaridhishwi nayo.
Wanafikiri labda kuna kitu hakipo sawa na hivyo wanaendelea kufanya zaidi na zaidi.
Lakini maisha yao ndiyo yanazidi kupotea zaidi.
Namna sahihi ya kuyaishi maisha yako ni hii; JUA MAANA YA MAFANIKIO KWAKO, KISHA FANYA YALE TU YANAYOKUFIKISHA KWENYE MAFANIKIO YAKO.
Usihangaike na kitu kingine chochote.
Hata kama kila mtu anafanya,
Kama hakichangii kwenye mafanikio yako, achana nacho.
Chochote ambacho hakina mchango wa kukufikisha kwenye mafanikio yako ni usumbufu kwako.
Hivyo ili ufanikiwe, ni lazima uondoe kila aina ya usumbufu kwenye maisha yako.
Kwenye maisha ni wachache sana wanaofanikiwa kwa sababu hao ndiyo wanaoweza kusimama wenyewe badala ya kufuata mkumbo.
Kuwa mmoja kati ya hao wachache, simama na kilicho sahihi kwako badala ya kuhangaika na usumbufu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu mambo yanayopoteza muda na nguvu zako, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/06/2106
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.