“There are three types of people. First, there are people who do not believe in anything; then, there are people who believe only in those teachings they were brought up to believe. Finally, there are people who believe in those things which they understand with their hearts, and this last group of people is the wisest and most resolute.” – Leo Tolstoy
Inapokuja kwenye imani, kuna aina tatu za watu.
Aina ya kwanza ni wale ambao hawaamini chochote na hawa maisha yao huwa magumu zaidi kwa kukosa kwao imani.
Aina ya pili ni wale ambao wanaamini kwenye yale mafundisho waliyokuzwa wakiamini.
Hawa huwa wanajiwekea ukomo kwenye imani zao na japo wanawazidi wasio na imani kabisa, hawa huwa hawafikii viwango vya juu.
Wanakuwa wanaamini kile tu walichopokea.
Aina ya tatu ni wale ambao wanaamini kile walichokielewa kwa mioyo yao wenyewe. Hawa wanakuwa wamejifunza, wakaelewa na kuchagua wenyewe kuamini.
Hawa ndiyo wanaofika ngazi ya juu kabisa ya hekima na hata kuweza kufanya makubwa.
Imani za watu hawa huwa hazina shaka na hawayumbishwi na chochote, kwa sababu hawajazipokea tu, bali wamezielewa na kuzikubali.
Kama bado, ingia kwenye kundi la tatu, chochote unachoamini, kielewe kwa kina na uchague mwenyewe kukiamini kutoka ndani ya moyo wako.
Usikubali tu kuamini kitu kwa sababu ndivyo kila mtu anavyoamini au unategemewa kuamini hivyo.
Maisha ni yako, una uhuru wa kuyaendesha kwa namna sahihi kwako na hilo linaanza na yale unayoamini.
Sehemu kubwa ya yale ambayo wengi kwenye jamii wanaamini siyo sahihi. Lakini wanayashikilia kwa sababu wamepoyapokea hivyo na yamewajengea hofu ya kutokuhoji au kuwa huru kujifunza na kuelewa kwa kina zaidi.
Sisi binadamu ni roho zilozo kwenye mwili,
Chakula cha roho ni yale unayoamini,
Chakula hicho kinakuwa na nguvu pale unapokuwa unakielewa vizuri kile unachokiamini.
Hivyo anza mara moja zoezi la kupitia yote unayoamini ili uhakikishe unayaelewa kwa kina.
Usiogope kubadili imani yako pale unapojifunza na kupata ambayo hukuwahi kupata.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kukimbilia kwenye vitabu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/07/2107
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.