“Do not pretend to understand something that you do not. It is one of the worst possible things to do.” – Leo Tolstoy
Kosa kubwa kabisa unaloweza kufanya kwenye maisha yako ni kijifanya unaelewa kile ambacho hukielewi.
Hilo ni kosa kwa sababu hutajifunza na hutaelewa.
Kama kuna kitu ambacho hujui, usione aibu kuuliza.
Kama kuna kitu hujaelewa, omba ufafanuliwe zaidi.
Kujifanya unajua na unaelewa hakutakupa kujua na kuelewa,
Badala yake kutapelekea uzidi kuwa mjinga.
Unapokiri hujui au hujaelewa, unakuwa mjinga mara moja na baada ya hapo unajifunza na kujua.
Unapojifanya unajua na kuelewa unakuea mjinga milele na hakuna unachojifunza.
Usiishi maisha ya maigizo, lengo la maisha yako siyo kujionesha au kuwafurahisha wengine, bali kuwa bora na kupiga hatua zaidi.
Usiruhusu chochote kiingilie mpango huo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kujiandaa kwa mchakato, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/08/2108
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.