Gharama ya ushauri wa bure utaiona pale utakapoanza kufanyia kazi ushauri huo. Watu wamekuwa hawaelewi uzito wa kauli hii, na hivyo wengi wameishia kuumizwa.

Na hakuna eneo ambalo ushauri wa bure umewagharimu wengi kama kwenye biashara. Wengi wameingia kwenye biashara kwa kufuata ushauri waliopewa bure na wengine lakini walipoanza kufanya biashara husika, ndiyo waligundua kwamba mambo siyo rahisi kama walivyokuwa wanachukulia awali.

Kuna aina nyingi za ushauri mbaya wa biashara ambazo zimewagharimu na kuwapoteza wengi, lakini leo nakwenda kukushirikisha aina moja ambayo ni maarufu na kila siku inawazamisha wengi.

Ushauri huo ni huu; BIASHARA FULANI INALIPA SANA, UKISHAKUWA NA MTAJI TU NA UKAINGIA KWENYE BIASHARA HIYO, MAFANIKIO NI UHAKIKA.

Kitu cha kwanza kinachopaswa kukupa tahadhari kwenye ushauri huu ni wanaoutoa huwa siyo wanaofanya biashara husika. Bali ni watu tu ambao wamekuwa wanaangalia wale wanaofanya biashara hiyo au washauri wa biashara ambao hawafanyi biashara husika.

Wengi wamekuwa wanapokea ushauri huo na kuwekeza mitaji yao kwenye biashara ambazo wameaminishwa zinalipa sana na hazitawasumbua kabisa. Lakini matokeo wanayokuja kuyapata yanakuwa ni tofauti.

Kwanza kabisa wanakutana na ushindani mkali ambao unawaweka kwenye hatari ya kushindwa, kwa sababu siyo wao tu wanakuwa wamepata ushauri huo, wengi wanakuwa wameusikia na kuufanyia kazi.

Pili wanakutana na changamoto ambazo ni kubwa na hawana maandalizi nazo. Walishaambiwa biashara hiyo haitawasumbua, ni kuweka mtaji na kuvuna faida, sasa wanapokutana na changamoto, inakuwa mshangao kwao.

Kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA unapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kupata wazo sahihi la biashara kwako. Kwenye sura ya kwanza kabisa ya kitabu hicho, unapata mchakato na hatua za kufuata ili kufika kwenye wazo ambalo litakuwa la kipekee kwako na ukilifanyia kazi utaweza kujenga biashara kubwa.

Kitabu hakiudanganyi kwamba kuna wazo rahisi na ambalo biashara haitakupa changamoto, bali kinakueleza wazi kwamba kila wazo la biashara lina ugumu na changamoto zake. Wazo utakalolipata kwa kufuata mchakato wa kitabu litakuwa la kipekee kwako, hivyo kuna changamoto mbalimbali utakazozipunguza.

Hata baada ya kulipata wazo lako la biashara, kitabu kitakusaidia kuliboresha wazo hilo ili kuondokana na changamoto zinazoweza kuwa kikwazo kwako baadaye.

Siyo kila biashara unayoona wengine wanafanya na wakafanikiwa basi na wewe ukiingia kuifanya utafanikiwa.

Siyo kila bidhaa au huduma ambayo wateja wanaulizia au wanaonekana kuitaka na kuikosa na ukaona unaweza kuiweka kwenye biashara yako italipa.

Kufanya maamuzi ya kibiashara kwa kufuata mkumbo au ushauri wa bure kumewagharimu wengi, usikubali wewe kuendelea kuwa kwenye kundi hilo.

Rafiki yangu mpendwa, nichukue nafasi hii kukujulisha kwamba kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kipo tayari kwa ajili yako. Ni kitabu kilichosheheni maarifa ya msingi kabisa ya biashara, yanayokuwezesha kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio makubwa.

Kitabu hicho kinakuwa mwongozo sahihi kwako katika kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara.

Gharama ya kupata kitabu ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sasa nakupa kama zawadi wewe rafiki yangu, utalipia tsh elfu 15 (15,000/=) tu kukipata kitabu hiki. Huu ni uwekezaji mdogo sana ambao ukiufanya, utaokoa fedha na muda wako unaopoteza kwa kufanya biashara isiyo sahihi kwako.

Kama bado hujaanza biashara, kitabu kitakusaidia kupata wazo sahihi kwako. Kama tayari upo kwenye biashara, kitabu kitakusaidia kuboresha wazo unalofanyia kazi sasa liwe sahihi kwako.

Karibu ujipatie nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA leo kabla zawadi hii hajamaliza muda wake. Wasiliana na 0752 977 170 kujipatia nakala yako sasa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Hiki ni kitabu kinachokuwezesha wewe kujua nguvu kubwa ya kutenda miujiza ambayo iko ndani yako.

Hapo ulipo sasa, tayari una nguvu kubwa sana ndani yako, ila hujaijua na wala hujaweza kuitumia.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kinakupa nafasi ya kujua nguvu hiyo na jinsi unavyoweza kuitumia.

Una uwezo wa kuwa chochote unachotaka, kufanya na kupata chochote unachotaka, lakini hiyo ni kama tu utaweza kutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.

Hakuna ambaye amewahi kukupa siri hii unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki, ni siri inayokwenda kuyafungua maisha yako na hakuna chochote kitakachofichwa tena kwako.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Zawadi hii ni ya muda mfupi na inakulenga wewe rafiki yangu, ambaye umekuwa unafuatilia mafunzo haya kwa muda mrefu, hivyo chukua hatua sasa kabla zawadi hii haijamaliza muda wake, wasiliana na 0752 977 170 na mwambie unataka zawadi ya vitabu vipya viwili; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA na UNA NGUVU YA KITENDA MIUJIZA na utapata nakala hizo.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania