“Any departure from accepted traditions and customs requires a large and serious effort, but true understanding of new things always requires such an effort.” – Leo Tolstoy

Kuachana na mazoea inakutaka mtu uweke jitihada na umakini mkubwa.
Kuacha kile ulichozoea kufanya na ambacho wengine wanafanya siyo rahisi.
Ndiyo maana wengi licha ya kujua kilicho sahihi kwao kufanya, bado huwa wanarudi kwenye mazoea.

Unapoanza kufanya tofauti, wale wanaofanya kwa mazoea hawatakuacha salama.
Watakushambulia, kukukosoa na kukukatisha tamaa.
Kama hujajitoa kweli kwamba unataka kubadilika, hutaweza kuvuka hayo.
Utaona ni bora kuenda na mazoea na kukubalika na wengine, kuliko kujaribu mapya na kupingwa.

Ni mmoja tu kati ya watu 100 ambayo huwa anafikis mafanikio makubwa,
Kwa sababu huyo ndiye aliyejitoa kweli kubadilika na kuwa tayari kukabiliana na chochote.
Na wewe unapaswa kuwa hivyo kama unataka kufikia mafanikio makubwa.

Ni kujidanganya kama unajiambia unataka mafanikio makubwa, huku ukiendelea kufanya yale uliyozoea.
Kama unataka mafanikio makubwa kweli, onesha hilo kwa kuwa tofauti kabisa na ulivyokuwa na hata walivyo wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu sababu za kufanya kilicho sahihi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/11/2111

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.