Ni kitu gani hasa unachokitaka kwenye maisha yako?

Kipi kinachokunyima usingizi na kila wakati unakifikiria?

Ninachotaka kukuambia na kukuhakikishia ni kwamba, chochote kile unachokitaka, uwezo wa kukipata uko ndani yako.

Haijalishi ni kitu kikubwa kiasi gani, ndani yako kuna nguvu kubwa ya kukuwezesha kukifikia.

Ila kwa bahati mbaya sana, nguvu hiyo imelala usingizi mzito na hivyo ni vigumu sana kwako kuweza kuitumia nguvu hiyo.

Kwa bahati nzuri sana, kuna njia unayoweza kuitumia kuamsha nguvu hizo kubwa zilizolala ndani yako, njia ambayo unaweza kuanza kuitumia mara moja na matokeo yakawa makubwa.

Njia hiyo ni kufanya tahajudi (meditation).

Wengi wanaposikia kufanya tahajudi huwa wanaona wamepotea kabisa, wanaona ni kitu kigumu na wasichoweza. Wengine huhusisha ufanyaji wa tahajudi na dini fulani.

Lakini hayo yote siyo kweli, kufanya tahajudi siyo kugumu na wala tahajudi siyo tu kwa ajili ya watu wa dini fulani. Tahajudi ni kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya na ikampa manufaa makubwa.

Lakini pia kuna tahajudi za aina nyingi, kwa kuwa lengo lako ni kupata unachotaka, kuna aina maalumu ya tahajudi ambayo inakupa unachotaka.

Aina hiyo inaitwa TAHAJUDI YA HATUA SITA. Hii ni tahajudi maalumu ambayo ina hatua sita za kufuata. Ukifanya tahajudi hii, unapata matokeo makubwa, unayoyaona na usiyoyaona.

Tahajudi ya hatua sita ni rahisi, inayohitaji kati ya dakika 15 mpaka 30 kufanya, lakini yenye matokeo makubwa mno kwenye maisha yako, kwa kuifanya kila siku unakuwa na siku tulivu na mawazo yako yanakuwa kwenye kile unachotaka na kwa umakini mkubwa, kitu kitakachokusaidia kufanikiwa sana.

Je ungependa kuijua kwa kina tahajudi hiyo ya hatua sita? Je ungependa kujua jinsi ya kufuata hatua hizo ili upate unachotaka? Je unataka kuwa na udhibiti zaidi kwenye maisha yako na jinsi siku zako zinavyokwenda?

Kama majibu ni ndiyo basi nikukaribishe usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Kwenye sura ya tatu ya kitabu hicho, unajifunza kwa kina kuhusu TAHAJUDI YA HATUA SITA na jinsi ya kufuata hatua hizo kwenye kuifanya.

Kitabu hicho pia kitakufundisha jinsi ya kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako, matokeo ambayo hujawahi kuyapata, ambayo tunayaita ni miujiza.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Kwa maisha yako yote, umekuwa unatamani kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, lakini hakuna ambaye amewahi kukupa mwongozo wa kufanya hivyo. Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kinakufunulia hilo, kipate na ukisome sasa ili usibaki hapo ulipo.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kwa hali inavyoenda, kwa ukosefu wa ajira uliopo na unaoendelea kukua, biashara ndiyo mkombozi pekee kwa kila mtu kuweza kuingiza kipato sahihi kwake.

Lakini wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kubahatisha, nasema hivyo kwa sababu watu hawaanzi na mawazo sahihi ya biashara, hawajui taratibu mbalimbali za kufuata na pia hawana mikakati ya kuiwezesha biashara kukua na kutokuwategemea.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimekuja na jawabu, kinakupa yale maarifa ya msingi kabisa ambayo kila mtu aliye kwenye biashara au anayepanga kuingia basi anapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi.

Hivyo kama tayari upo kwenye biashara au unapanga kuingia kwenye biashara, pata nakala yako leo ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ili uweze kujenga biashara yako kwenye misingi sahihi na ufanikiwe.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini leo ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 pekee. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania