“The great thing in this world is not so much where we stand as in what direction we are moving.” – Oliver Wendell Holmes Sr.
Jambo muhimu zaidi kwenye maisha yako siyo pale uliposimama sasa, bali kule unakoelekea.
Haijalishi kwa sasa uko wapi, kama upo kwenye uelekeo sahihi, utafika mahali sahihi.
Wengi hupoteza muda kulalamikia pale walipo sasa, badala ya kuhangaika kuwa kwenye uelekeo sahihi utakaowatoa pale walipo.
Uzuri wa maisha ni kila kitu huwa kinabadilika, hakuna kinachobaki kilivyo milele.
Kama utajua wapi unapotaka kufika na kisha kupambana kupiga hatua za kufika huko, maisha yako yatakuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.
Usikatishwe tamaa na pale ulipo sasa, kazana kupiga hatua zaidi na utapata matokeo yaliyo bora zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kufanya kitu kuwa bora zaidi ya kilivyo sasa, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/13/2113
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.