“Amateurs sit and wait for inspiration, the rest of us just get up and go to work.” – Stephen King

Kitu kikubwa kinachowatofautisha wabobezi na wachanga ni hamasa.
Wachanga huwa wanasubiri hamasa ije ndiyo waanze kufanya. Na kwa sababu hamasa haitabiriki wala haitegemeki, huwa wanachelewa kuanza kufanya na hivyo hawafanyi makubwa.

Wabobezi huwa wanapanga nini wanataka kufanya, wakati gani watafanya na ukishafika wakati wanaanza kufanya kama walivyopanga, iwe wana hamasa au la.
Kwa namna hii kila wakati wanakuwa wanafanya na hilo linawawezesha kufanya makubwa sana.

Asubuhi ya leo jitafakari ni kitu gani umekuwa unapanga kufanya lakini huanzi kufanya. Kila unapotaka kuanza unakosa hamasa au ukianza hufiki mbali maana hamasa inaisha haraka.
Chagua kitu kimoja na andika mahali unataka kufanya NINI, utafanya WAKATI gani, UTAFANYAJE na utafanyia WAPI. Kisha tekeleza mpango wako kama ulivyoweka.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu rasilimali tano muhimu unazopaswa kulinda sana, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/14/2114

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani