Kikwazo cha wengi kuingia kwenye biashara kimekuwa ni mtaji, hiki kimekuwa kilio cha kila anayetaka kuingia kwenye biashara na akashindwa au aliye kwenye biashara na kushindwa kuikuza.

Kila anayeshindwa kuingia kwenye biashara au aliye kwenye biashara na kushindwa kuikuza, sababu yake kuu huwa ni kukosa mtaji.

Lakini mimi nimekuwa nawaeleza watu ukweli huu; kukosa mtaji hakujawahi kumzuia mtu mwenye nia ya kweli kuingia kwenye biashara. Bali kukosa mtaji ni sababu rahisi kwa yeyote kutumia, ambayo hakuna anaweza kukukatalia.

Naamini kutoka ndani yangu, bila ya shaka yoyote kwamba mtu yeyote anaweza kuanzisha na kukuza biashara yake hata kama hana kabisa mtaji wa kuanzisha biashara hiyo.

Nina ushahidi kwangu binafsi na ushahidi kutoka kwa wengine wa jinsi gani hilo linawezekana.

Na leo nakupa nafasi ya wewe kujua hili, ili uache kutoa visingizio na uanzishe au kukuza biashara yako.

AINA ZA MITAJI.

Watu wengi wanapozungumzia mtaji wa biashara, huwa wanazungumzia aina moja tu ya mtaji, ambayo ni mtaji fedha. Wakikosa aina hii ya mtaji, wanaona hawawezi kuingia kwenye biashara.

Usichojua ni kwamba kuna aina tano za mtaji wa kuanzisha biashara, fedha ni moja ya aina hizo, ila kuna aina nyingine 4 ambazo ukijua jinsi ya kuzitumia vizuri utaweza kuanzisha biashara.

Ninachotaka kukuambia hapa ni kwamba, hata kama huna fedha, kuna aina nyingine za mtaji unazo katika hizo tano, hivyo usikate tamaa na kujiambia kwa kuwa huna mtaji basi huwezi kuingia kwenye biashara.

Kwenye kitabu kipya nilichoandika cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA nimeelezea kwa kina aina hizo tano za mtaji na jinsi unavyoweza kuanza nazo biashara. Pata nakala yako ya kitabu leo, kwa maelezo nitakayotoa hapo chini na ujifunze na kuingia kwenye biashara mara moja.

VYANZO VYA MTAJI FEDHA.

Inapokuja kwenye mtaji fedha, wengi wanaokwama kupata mtaji huu huwa wanahangaika na njia moja tu, na wengi ni njia ya mkopo. Utawasikia wengi wakisema sina sifa ya kukopesheka, hivyo siwezi kupata mtaji wa kuanza biashara.

Hili pia siyo sahihi, kwa sababu vyanzo vya mtaji wa fedha siyo mkopo pekee.

Kuna vyanzo vikubwa vitano vya kupata mtaji wa fedha kwenye biashara, mkopo ni moja kati ya njia hizo tano na ambao una vikwazo vingi.

Kuna vyanzo vingine vya kupata mtaji fedha, tena ambavyo ni rahisi na visivyokuumiza kama kilivyo chanzo cha mkopo. Ulivijua vyanzo hivyo na jinsi ya kuvitumia vizuri, utaweza kupata fedha za kuanzisha na kukuza biashara yako ambapo hulazimiki kulipa riba kubwa.

Kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, unapata nafasi ya kujua vyanzo hivyo mbadala vya mtaji fedha kwenye biashara na jinsi ya kuvitumia kuweza kuanzisha na kukuza biashara yako.

Rafiki yangu mpendwa, jipatie leo nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, uweze kupata mafunzo sahihi yatakayokuwezesha kuanzisha na kukuza biashara yenye mafanikio makubwa. Hiki ni kitabu kilichosheheni maarifa ya msingi kabisa ya biashara, ambayo hukupata nafasi ya kufundishwa popote pale. Kwa kuwa na maarifa haya, hutayumbishwa kibiashara.

Kitabu hiki ni mwongozo sahihi kwako katika kufikia mafanikio makubwa kwenye biashara.

Gharama ya kupata kitabu ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sasa nakupa kama zawadi wewe rafiki yangu, utalipia tsh elfu 15 (15,000/=) tu kukipata kitabu hiki. Huu ni uwekezaji mdogo sana ambao ukiufanya, utaokoa fedha na muda wako unaopoteza kwa kufanya biashara isiyo sahihi kwako.

Kama bado hujaanza biashara, kitabu kitakusaidia kupata wazo sahihi kwako. Kama tayari upo kwenye biashara, kitabu kitakusaidia kuboresha wazo unalofanyia kazi sasa liwe sahihi kwako.

Karibu ujipatie nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA leo kabla zawadi hii hajamaliza muda wake. Wasiliana na 0752 977 170 kujipatia nakala yako sasa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Hiki ni kitabu kinachokuwezesha wewe kujua nguvu kubwa ya kutenda miujiza ambayo iko ndani yako.

Hapo ulipo sasa, tayari una nguvu kubwa sana ndani yako, ila hujaijua na wala hujaweza kuitumia.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kinakupa nafasi ya kujua nguvu hiyo na jinsi unavyoweza kuitumia.

Una uwezo wa kuwa chochote unachotaka, kufanya na kupata chochote unachotaka, lakini hiyo ni kama tu utaweza kutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.

Hakuna ambaye amewahi kukupa siri hii unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki, ni siri inayokwenda kuyafungua maisha yako na hakuna chochote kitakachofichwa tena kwako.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Zawadi hii ni ya muda mfupi na inakulenga wewe rafiki yangu, ambaye umekuwa unafuatilia mafunzo haya kwa muda mrefu, hivyo chukua hatua sasa kabla zawadi hii haijamaliza muda wake, wasiliana na 0752 977 170 na mwambie unataka zawadi ya vitabu vipya viwili; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA na UNA NGUVU YA KITENDA MIUJIZA na utapata nakala hizo.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania