“In the world people take a man at his own estimate; but he must estimate himself at something. Disagreeableness is more easily tolerated than insignificance.” – Johann Wolfgang von Goethe
Watu huwa wanakuchukulia kwa namna unavyojichukulia wewe mwenyewe.
Kama unajiheshimu basi pia watu watakuheshimu.
Na kama unajidharau na wao pia watakudharau.
Huhitaji kuwalazimisha watu wakuchukulie kwa namna fulani, anza kujichukulia hivyo wewe mwenyewe na wengine watafuata.
Katika kujiwekea viwango vyako mwenyewe, usiogope watu kutofautiana na wewe.
Ni heri watu wasikubaliane na wewe kuliko wakupuuze kabisa.
Hivyo jiwekee viwango, ambavyo utaviishi na kuvisimamia na wengine watalazimika kuvifuata hivyo pia.
Kuwa wewe na ishi maisha yako, wengine watajipanga jinsi ya kuendana na wewe.
Asubuhi ya leo tafakari ni namna gani watu wamekuwa wanakuchukulia na je unapenda namna hiyo?
Kama jibu ni hapana, jiulize ni namna gani ungependa watu wakuchukulie, kisha anza kujichukulia hivyo wewe mwenyewe.
Haitachukua muda watu wataanza kukuchukulia hivyo.
Na kama kuna watakaokuambia siku hizi umebadilika au kukupinga kwa namna mpya unayojichukulia, basi jua dawa imefanya kazi na usilegeze.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kizazi laini laini cha zama hizi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/16/2116
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.