Kama kufanya kazi kwa juhudi pekee ndiyo lingekuwa hitaji la kupata mafanikio na utajiri, basi punda wangekuwa ndiyo wanyama wenye mafanikio makubwa kuliko wote, lakini siyo.

Na hata kwetu sisi binadamu, masikini wanafanya kazi ngumu na kwa muda mrefu, lakini bado wanabaki kwenye umasikini wao.

Na hapa siyo swala la kufanya kazi kwa nguvu (work hard) au kufanya kazi kwa akili (work smart), bali ni zaidi ya hapo.

Wale wanaopata fedha na mafanikio makubwa kwenye maisha yao, wana kitu cha ziada, zaidi ya kuweka akili na nguvu kwenye kazi zao.

Wanajua nguvu ya miujiza iliyo ndani yao na jinsi ya kuitumia kuvuta fedha na mafanikio kuja kwao. Pamoja na kuweka juhudi kubwa na akili kwenye kazi, lakini pia wanaitumia nguvu ya miujiza na hapo wanavutia matokeo makubwa kuja kwao.

Kwa wale wasioelewa kuhusu nguvu hii, ambayo ipo ndani ya kila mmoja wetu, huamini wale wanaopata fedha nyingi na kufanikiwa sana wana namna ya ziada. Wengi huonekana kama wanatumia nguvu za kishirikina au majini na kupewa majina mbalimbali.

Wasichojua wengi ni kwamba watu hao hawana ushirikina wowote, wala majini, wala chochote cha ziada ambacho wengine hawana. Bali watu hao wana utambuzi wa nguvu kubwa iliyo ndani yao na wanajua jinsi ya kuitumia kufanya makubwa.

Wale wanaojua kuhusu nguvu hiyo ya miujiza, wengi walikutana nayo kwa bahati tu na wala hawajui kama ndiyo inawasaidia, hivyo hawawezi kuwafundisha wengine kuhusu nguvu waliyonayo wao na jinsi wanavyoitumia.

Ndiyo maana kwa muda mrefu, wachache sana ndiyo wamekuwa wanafanikiwa huku wengi wakibaki kwenye hali ya chini.

Lakini hilo halipaswi kuendelea tena, hasa kwako wewe afiki yangu, kwa sababu siri hiyo iliyokuwa imefichwa, sasa iko wazi. Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kinakupa nafasi ya kutambua nguvu kubwa iliyo ndani yako na jinsi unavyoweza kuitumia kufanya makubwa.

Moja ya makubwa unayoweza kufanya na nguvu iliyo ndani yako, ni kuvuta fedha zije kwako. Kwenye ukurasa wa 127 wa kitabu, kuna hatua tano za kufuata ambazo zitavuta fedha zije kwako. Ni hatua rahisi ambazo ukizielewa na kuzifanyia kazi halafu ukaendelea kuweka nguvu na akili kwenye kila unachofanya, hakuna kitakachoweza kukuzuia usipate kiwango chochote cha fedha unachotaka kupata.

Jipatie leo nakala yako ya kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uitambue nguvu iliyo ndani yako na jinsi ya kuitumia kuvuta fedha na mafanikio makubwa kuja kwako.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Kwa maisha yako yote, umekuwa unafichwa siri ambayo iko mbele ya macho yako, ni wakati sasa wa kufichua siri hiyo ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako na upate mafanikio makubwa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kwa hali inavyoenda, kwa ukosefu wa ajira uliopo na unaoendelea kukua, biashara ndiyo mkombozi pekee kwa kila mtu kuweza kuingiza kipato sahihi kwake.

Lakini wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kubahatisha, nasema hivyo kwa sababu watu hawaanzi na mawazo sahihi ya biashara, hawajui taratibu mbalimbali za kufuata na pia hawana mikakati ya kuiwezesha biashara kukua na kutokuwategemea.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimekuja na jawabu, kinakupa yale maarifa ya msingi kabisa ambayo kila mtu aliye kwenye biashara au anayepanga kuingia basi anapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi.

Hivyo kama tayari upo kwenye biashara au unapanga kuingia kwenye biashara, pata nakala yako leo ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ili uweze kujenga biashara yako kwenye misingi sahihi na ufanikiwe.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini leo ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 pekee. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania