“Whatever we plant in our subconscious mind and nourish with repetition and emotion will one day become a reality” — Earl Nightingale

Watu huwa wanayalalamikia maisha yao wakiamini kuna watu wamepelekea wao kufika pale walipo sasa.
Lakini ukweli ni kwamba popote mtu alipo, ni mavuno ya kile alichopanda kwenye fikra zake siku za nyuma.
Haupo hapo ulipo sasa kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya fikra ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu.

Wazo lolote utakalolipanda kwenye fikra zako na kulirutubisha kwa kurudia rudia na hisia, siku moja linakuja kuwa uhalisia.
Kile mtu anachopata siyo bahati wala ajali, bali mavuno ya kile ambacho amekipanda na kukipalilia kwa muda mrefu.

Asubuhi ya leo tafakari ni mawazo gani yamekuwa yanatawala fikra zako kwa muda mrefu. Ni mawazo gani umekuwa unayarudia rudia kwa hisia kali. Jua hiyo ni mbegu ya maisha yako yajayo.
Pata picha ya kule unakotaka kufika na kuwa na fikra hizo kila mara, huku ukizipa hisia ya kujiona kama tayari umeshafika unakotaka kufika.

Kwa kuwa lazima utafikiri, kwa nini usifikiri mawazo bora na makubwa ili upate matokeo bora na makubwa?

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kufanya bure kuliko kutokufanya kabisa, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/10/23/2123

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.