Rafiki yangu mpendwa,

Nilipoanza kuandika kwenye blog ya AMKA MTANZANIA mwaka 2013, hakukuwa na blog nyingi zinazoweka makala za mafunzo. Blog zilizoeleka kuwa za mambo ya udaku na habari mbalimbali.

Wapo waliojitolea kunipa ushauri kwamba ‘Watanzania siyo watu wa kusoma mambo chanya mtandaoni, ni watu wa kufuatilia mambo ya udaku.’ Nilichowajibu ni kimoja, mimi napenda kusoma na kujifunza mambo haya chanya, siwezi kuwa mwenyewe nchi nzima, wapo wanaopenda pia ila hawajajua pa kuyapata.

Hivyo niliendelea kuandika licha ya kuwa na wasomaji wachache na wengi kuwa wakatishaji tamaa. Na leo hii nimeweza kuwa na wasomaji wengi.

Kitu kikubwa sana ninachokiheshimu na siwezi kukisahau ni wasomaji wa mwanzo kabisa, walioniamini wakati naanza uandishi na mpaka sasa wapo na mimi. Hawa ni watu ninaowathamini mno. Na ndiyo maana kila ninapotoa vitabu au huduma nyingine huwa siwasahau watu hao walioniamini tangu awali.

Na ndiyo maana kwenye vitabu vipya viwili nilivyotoa sasa, kwa kipindi hiki cha mwanzo nimevitoa kwa bei ya zawadi, ili kuhakikisha marafiki zangu ambao wamekuwa na mimi kwa muda mrefu hawakosi maarifa haya ninayoyatoa.

Vitabu vipya nilivyotoa ni UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA na ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ambavyo kwa sasa unavipata kwa bei ya zawadi ya Tsh elfu 15 kwa kila kimoja badala ya tsh elfu 20 kwa kila kimoja.

Ninachopenda kukuambia rafiki yangu ni kwamba zawadi hii inaisha ndani ya siku 7 zijazo, yaani tarehe 30/10/2020, hivyo kama bado hujachukua hatua, chukua sasa ili usikose zawadi hii.

Nakupenda na kukuthamini sana rafiki yangu, kwa kuwa tumekuwa pamoja kwenye safari hii, nimekuwa nakazana kukuandalia maarifa yanayokuwezesha kupiga hatua na pia kuhakikisha huyakosi kwa sababu yoyote ile. Wahi bei hii ya zawadi kwa vitabu hivi vipya ili usikose maarifa haya bora ya kukuwezesha kufanikiwa zaidi.

Maelezo mafupi ya vitabu hivyo vipya ni kama ifuatavyo;

KITABU; UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

Kila mtu amewahi kusikia au  kuona miujiza ikitokea kwake au kwa wengine. Sehemu kubwa ya miujiza hiyo huwa inafanywa na watu wengine. Mfano ni pale mtu anapofanyiwa maombi na kisha akapona ugonjwa fulani au kupata matokeo fulani mazuri.

Kitu ambacho umekuwa huelezwi na wewe mwenyewe hujajua ni kwamba miujiza yoyote ile huwa inaanzia ndani ya mtu na siyo kutoka nje yake. Wale wa nje wanaoonekana kusababisha miujiza, huwa tu wanamsaidia mtu kufikia kwenye miujiza hiyo.

Ninachokueleza hapa rafiki yangu ni hiki, wewe hapo ulipo, una nguvu na uwezo mkubwa wa kutenda miujiza kwenye maisha yako.

Ndiyo, umesikia vizuri, wewe wewe, pamoja na yote yanayoendelea kwenye maisha yako, nguvu ya miujiza ipo ndani yako.

Lakini kwa bahati mbaya sana, hakuna ambaye amewahi kuchukua hatua kukujulisha kuhusu nguvu hii iliyopo ndani yako. Ndiyo maana huijui na hujaweza kuitumia.

Sasa umepata bahati ya kipekee sana ya kuweza kuijua nguvu ya kutenda miujiza iliyo ndani yako, na jinsi unavyoweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yako.

Kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, kinakupa nafasi ya kujua nguvu hiyo na jinsi unavyoweza kuitumia.

Una uwezo wa kuwa chochote unachotaka, kufanya na kupata chochote unachotaka, lakini hiyo ni kama tu utaweza kutambua na kutumia nguvu kubwa iliyo ndani yako.

Hakuna ambaye amewahi kukupa siri hii unayokwenda kujifunza kwenye kitabu hiki, ni siri inayokwenda kuyafungua maisha yako na hakuna chochote kitakachofichwa tena kwako.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa. Mwisho wa bei ya zawadi ni tarehe 30/10/2020, chukua hatua sasa ili usiikose.

ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Biashara fulani inalipa kweli, wewe ifanye tu na utapata mafanikio, huu ni moja ya ushauri ambao umewapoteza wengi kibiashara.

Wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kufuata mkumbo au ushauri wa bure kama huo na kuishia kupoteza mtaji na muda wao.

Biashara zimekuwa changamoto kwa wengi kwa sababu hakuna elimu sahihi inayotolewa kuhusu biashara.

Kwenye elimu ya msingi ambayo kila mtu anajifunza yale ya msingi kwenye maisha, biashara siyo moja ya misingi inayofundishwa.

Na hata wale wanaokwenda kusomea masomo ya biashara wanachojifunza ni vitu vinavyohusu biashara, mfano mlolongo wa thamani (chain of value), uhitaji na upatikanaji (demand and supply) na kutunza vitabu (book keeping).

Lakini kupata mafunzo kamili ya biashara, kuanzia kupata wazo sahihi, kugeuza wazo hilo kuwa biashara inayojiendesha kwa faida na kuweza kuiendesha biashara hiyo mpaka kufikia mafanikio, ni elimu ambayo hakuna inakopatikana.

Kwa kuona ombwe hili na changamoto ambazo wengi wanakutana nazo kwa kutokuijua misingi ya biashara, nimefanya utafiti wa kina na kutumia uzoefu wangu na wa watu wengine na kuweza kuja na kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Hii ni elimu ya msingi kweli kwa sababu ina yote muhimu ambayo mtu anapaswa kuyajua kuhusu biashara. Kuanzia kupata wazo, kusajili biashara, kutengeneza thamani, kupata wateja, kuwahudumia vizuri, kuajiri watu sahihi na hata kuikuza zaidi biashara yako.

Kwa zama tunazoishi sasa, ambapo nafasi za ajira ni chache kuliko wanaozihitaji, biashara ndiyo mkombozi. Lakini kwenda kuingia kwenye biashara kichwa kichwa bila ya kuijua misingi, ni kujipeleka kwenye anguko.

Pata leo nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, kama upo kwenye biashara utaweza kuiendesha biashara yako vizuri na kama ndiyo unapanga kuingia basi utajua yale muhimu ya kuzingatia ili ufanikiwe.

Bei ya kitabu hiki ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kama nilivyokueleza kwenye makala hii, nakwenda kukupa zawadi. Hivyo leo utakipata kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa. Mwisho wa bei ya zawadi ni tarehe 30/10/2020, chukua hatua sasa ili usiikose.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Nikukumbushe kwamba mwisho wa zawadi hii ni tarehe 30/10/2020, baada ya hapo vitabu vitakuwa vinapatikana kwa bei yake halisi. Chukua hatua leo hii ili usikose zawadi hizo nzuri kwako rafiki yangu.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania