“It is not enough to know, we must also apply; it is not enough to will, we must also do.” – Johann Wolfgang von Goethe
Kujua pekee haitoshi, ni lazima uweke kwenye matendo kile unachojua ndiyo uweze kunufaika nacho.
Hekima ni kuweka kwenye matendo maarifa unayoyapata.
Haijalishi unajua kiasi gani, kama unachofanya hakiendani na unachojua, maarifa uliyonayo ni mzigo kwako.
Kwa kila unachojifunza, ondoka na hatua unazokwenda kuchukua ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usijisifie ni vitabu vingapi umemaliza, bali angalia usomaji wa vitabu umeyabadili vipi maisha yako.
Kwa kila kitabu unachosoma, ondoka angalau na kitu kimoja unachokwenda kufanyia kazi kwenye maisha yako.
Kutaka mafanikio makubwa pekee haitoshi, ni lazima uchukue hatua ili kufikia mafanikio hayo.
Wengi huweka malengo na mipango mizuri kabisa, lakini hawachukui hatua zozote za tofauti.
Wanafikiri kuna muujiza utatokea wa kupata wanachotaka bila kuchukua hatua.
Miujiza inaweza kutokea sana kwenye maisha yako, ila inatokana na hatua ambazo mtu unachukua.
Kama hupigi hatua kwenye maisha yako usitafute wa kulaumu, bali angalia nini hufanyi.
Maana kinachokukwamisha ni hatua ambazo huchukui.
Kwa kila unachojifunza, kiweke kwenye matendo.
Kwa kila unachotaka, chukua hatua ili kukipata.
Hakuna ugumu wowote kwenye mambo haya mawili, lakini yamewakwamisha wengi sana.
Usikubali yaendelee kukukwamisha na wewe pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wakati sahihi wa kuyaamini machale yako, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/11/2142
Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.