“At all times it has not been the age, but individuals alone, who have worked for knowledge. It was the age which put Socrates to death by poison, the age which burnt Huss. The ages have always remained alike.” – Johann Wolfgang von Goethe
Mabadiliko yote ambayo yamewahi kutokea hapa duniani na yakawa na manufaa sana, yote yamekuwa yanaletwa na mtu mmoja mmoja na siyo kundi.
Ugunduzi wa kisayansi, teknolojia mpya na njia bora za kufanya mambo, yote hayo yameletwa na mtu mmoja mmoja.
Kazi kubwa ya kundi ni kulinda mazoea, kuhakikisha kila kitu kinaendelea kuwa kama kilivyo.
Ukilifuata kundi, kwa hakika utaendelea kufanya yale yanayofanyika.
Manadiliko pekee ambayo yamekuwa yanasababishwa na kundi ni mabaya.
Mauaji, vita na mafarakano mbalimbali, huwa ni matokeo ya kundi kutaka kubali lilivyo na kukataa kuelewa au kukubaliana na kundi jingine.
Kama unataka kuwa na maisha ya mafanikio,
Kama unataka kuleta mabadiliko kwako binafsi na kwa wengine pia,
Ni lazima uwe tayari kusimama mwenyewe na kwenda tofauti na kundi.
Hilo halitakuwa rahisi kwa sababu kundi halitakuacha ufanye unavyotaka,
Litakulazimisha urudi kwenye mazoea ya kundi, kwa kukupiga, kukutisha na kukukatisha tamaa.
Ni lazima uwe umejitoa kweli na uwe tayari kusimama imara kwa gharama yoyote ile.
Enzi za Galileo, kundi zima liliamini jua linazunguka dunia.
Galileo akafanya tafiti mbalimbali, akaja na ushahidi ulio wazi kwamba dunia ndiyo inalizunguka jua.
Kundi likakataa, likamfunga na kumuua Galileo.
Leo hii tunamjua Galileo na kujifunza kwake, waliokuwa kwenye kundi wamesahaulika kabisa.
Hata kama kundi litakupinga na kukuwekea vikwazo kiaso gani,
Jua mwisho wa siku mabadiliko unayoleta yanaacha alama kubwa kwako na vizazi vijavyo.
Usikubali kukatishwa tamaa na kundi,
Jua kundi haliwezi kuleta mabadiliko mazuri,
Hivyo pambana kusimama mwenyewe kwenye kile unachojua ni sahihi,
Huku ukiongozwa na nguvu na imani kuu ya upendo, kwako mwenyewe, kwa wengine na kwa kile unachofanya.
Ukishakuwa na upendo wa kweli kabisa, usiogope kusimamia chochote, hata kama jamii inakupinga kiasi gani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kulipa sasa au kulipa baadaye, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/21/2152
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante sana kocha kwa tafakari, hakika kundi linaishi kwa mazoea, Mabadiliko ninayohitaji lazima niwe tayari kusimamia MALENGO yangu bila kujali kundi linasemaje.
LikeLike
Vizuri Beatus.
LikeLike