“Those who are not grateful soon begin to complain of everything.” — Thomas Merton

Watu wanaolalamikia kila kitu kwenye maisha yao, ni watu ambao hawana shukrani.
Ukiwa mtu wa shukrani, kuna mambo mengi ya kushukuru kwenye maisha kuliko kulalamika.
Hata pale unapokutana na magumu, ukiwa mtu wa shukrani, hutakosa cha kushukuru kwenye magumu hayo uliyokutana nayo.

Unapokuwa mtu wa shukrani unatafuta uzuri kwenye kila hali unayopitia.
Na kwenye maisha, huwa tunapata kile tunachotafuta.
Ukitafuta cha kulaumu lazima utakipata.
Kadhalika ukitafuta cha kushukuru pia utakipata.

Kuwa mtu wa shukrani, shukuru kwa kila jambo na hilo litakupelekea wewe kuziona fursa nyingi na nzuri kwako.
Usiwe mtu wa kulalamika na kulaumu wakati wote,
Kuwa mtu wa shukrani na kwenye kila hali unayopitia utayaona mazuri na kuweza kunufaika zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kurudia rudia, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/23/2154

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.