“When we love, we always strive to become better than we are. When we strive to become better than we are, everything around us becomes better too.”
— Paulo Coelho
Unapopenda, unakazana kuwa bora kuliko ulivyokuwa awali.
Unapokazana kuwa bora, kila kinachokuzunguka kinakuwa bora pia.
Hivyo njia rahisi ya kubadili kitu chochote au mtu yeyote ni upendo.
Watu wengi wamekuwa wanajiambia wanataka kuibadili dunia au kuwabadili watu wengine.
Wanaweka nguvu kubwa kuhakikisha wanaleta mabadiliko,
Lakini hawafanikiwi, kuleta mabadiliko.
Dunia ni ngumu (complex) na watu hawatabiriki.
Unapoweka nguvu kwenye kuleta mabadiliko yoyote yale, nguvu hizo zinarudi kwako zikiwa na ukinzani mkali.
Lakini unapotumia upendo, mabadiliko yanatokea bila ya kutumia nguvu kubwa.
Kwa sababu unapopenda kitu au mtu kweli, unakazana wewe mwenyewe kuwa bora na ukishakuwa bora, kila kinachokuzunguka kinakuwa bora.
Kwa lugha nyingine tunaweza kusema njia ya kubadili chochote kile ni kwa kuanza kubadilika wewe mwenyewe.
Usipobadilika, hakuna kinachobadilika.
Na kubadilika wewe mwenyewe ni kugumu sana kama hujakipenda kweli kitu.
Kwa kuwa mabadiliko ni magumu hata kwetu binafsi na upendo unarahisisha mabadiliko, basi upendo ndiyo nguzo kuu ya mabadiliko.
Kama kuna kitu au mtu unataka kumbadili, acha kutumia nguvu na anza kutumia upendo.
Kwa upendo na kujipa muda, hakuna mabadiliko yanayoshindikana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu ya kila mtu haina mtu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/25/2156
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.