“It is better, however, to get no return than to confer no benefits. Even after a poor crop one should sow again; for often losses due to continued barrenness of an unproductive soil have been made good by one year’s fertility.” – Seneca

Mkulima wa kweli, ambaye ameyatoa maisha yake kwa ajili ya kilimo, huwa haachi kupanda kwa sababu msimu uliopita hakuvuna.
Ataendelea kupanda kwa sababu anajua hata kama msimu uliopita alikosa, haimaanishi na msimu huu pia atakosa.
Anajua wajibu wake ni kupanda mbegu na kuzitunza vizuri, anautekeleza.

Mfanyabiashara wa kweli, ambaya amejitoa kweli kuifanya biashara, haachi biashara kwa sababu amepata hasara.
Anajua hasara ni sehemu ya biashara na wajibu wake ni kukazana kufanya kilicho sahihi.

Wanaoteseka na kusumbuka kwenye maisha, ni wale wanaoendesha maisha kwa majaribio.
Ambao hawajajitoa kweli kufanya kitu walichochagua kufanya.
Hao ni wale wanaosikia kilimo fulani kinalipa kweli kweli, wanakimbilia kwenda kukifanya, wanapata hasara na wanaachana nacho.
Wale wanaoambiwa biashara fulani inalipa sana, wanaingia, wanapata hasara, wanakimbia haraka mno.

Wanaofanikiwa wanakua hili, kilicho ndani ya uwezi wao ni hatua wanazochukua, matokeo hayapo ndani ya uwezo wao.
Hivyo wamejitoa kuchukua hatua, bila ya kujali ni matokeo gani wanapata.
Kwa kila matokeo wanayopata wanajifunza na kujiboresha zaidi.

Mimi nilishachagua kuandika, kutibu na kukochi ni vitu nitakavyofanya bila ya kuacha, hata kama matokeo yatakuwaje.
Je wewe ni kitu au vitu gani umechagua kwa namna hiyo?
Tushirikishe hapa ili iwe ahadi kwa kila mmoja wetu.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu vyote kwa pamoja, kipato na matumizi, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/11/26/2157

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.