“Even Socrates, Cato, and Laelius might have been shaken in their moral strength by a crowd that was unlike them; so true it is that none of us, no matter how much he cultivates his abilities, can withstand the influence of their surroundings. Associate with those who will make a better man of you.” – Seneca
Huwa tunajidanganya kitu kimoja,
Kwamba tunaweza kuzungukwa na watu wa aina fulani, lakini tusiige tabia zao, yaani tukabaki na tabia zetu.
Huko ni kujidanganya kwa sababu hakuna mwenye uwezo huo.
Hata wanafalsafa waliokuwa na misingi na misimamo waliyoiishi, hawakuwa na uwezo wa kuepuka ushawishi wa wale wanaowazunguka.
Hivyo dawa ni moja tu, waepuke kama ukoma wale ambao hutaki kuwa kama wao.
Kabla hujajihusisha na yeyote, angalia tabia zake, angalia maisha yake.
Jua kwa kujihusisha naye, utaishia kuwa na tabia kama zake na maisha kama yake.
Haijalishi u mjanja kiasi gani, au unajiambia huwezi kushawishika.
Ukishakuwa na ukaribu na mtu au watu, tabia zao moja kwa moja zinakuingia, bila hata ya kujua.
Kwa zama hizi hilo linakwenda mbali zaidi na kuhusisha wale unaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii au kusoma kazi zao.
Hata kama wako mbali, kwa kuwafuatilia kwa muda mrefu, unaishia kuwa kama wao, kitabia na kimaisha.
Hivyo kuwa makini sana na wale unaochagua kuwafuatilia kwenye mitandao au kwa njia nyingine.
Jihusishe na watu ambao wanakufanya uwe bora zaidi ya ulivyo sasa.
Na watu hao wanapaswa kuwa tayari ni bora au wanapambana kuwa bora.
Kama kuna tabia au aina ya maisha ambayo mtu anayo na usingependa kuwa nayo, muepuke sana mtu huyo
Kwa kuwa na ukaribu naye utaishia kuwa kama yeye.
Hakuna mwenye nguvu ya kushinda ushawishi wa watu wanaokuwa karibu yake.
Hivyo chagua kwa umakini sana ni watu gani unaokuwa karibu nao.
Hakikisha ni watu wanaokufanya uwe bora zaidi ya ulivyo sasa.
Na wewe pia hakikisha unakuwa mtu sahihi kwa wengine, kwa kuwasaidia wawe bora zaidi ya walivyo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu kiburi na ujinga, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/03/2164
Rafiki yako anayekupenda sana na anayetaka uwe bora zaidi ya ulivyo sasa,
Kocha Dr Makirita Amani.