“In order to discover one grateful person, it is worth while to make trial of many ungrateful ones.” – Seneca

Huwa tunajiwekea mipango mbalimbali, ambayo huwa haijumuishi changamoto tunazoweza kukutana nazo.
Lakini kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho ni kwamba changamoto huwa hazikosekani.
Tunataka kila kitu kiende kama tunavyotaka sisi, lakini hivyo sivyo dunia inavyokwenda.

Kabla hujafikia mtu au kitu sahihi kwako, lazima upite kwa wengi na vingi ambavyo siyo sahihi.
Kabla hujapata mtu sahihi wa kushirikiana naye, utapita kwa wengi ambao siyo sahihi.
Kabla hujapata wafanyakazi wazuri wa kukusaidia, utapita kwanza kwa wasio sahihi.
Kabla hujakutana na kazi au biashara nzuri ya kufanya, lazima utapitia ambazo siyo nzuri.

Hivyo usiwe mtu wa kukata tamaa haraka pale ambapo mambo hayaendi kama ulivyopanga.
Kwa sababu umekutana na watu kumi wasio sahihi, haimaanishi hakuna watu sahihi, dunia ina watu zaidi ya bilioni 7, hujawamaliza wote.

Ukibahatika kupata kilicho sahihi kwa mara ya kwanza vizuri, lakini usikate tamaa pale unapokutana na yasiyo sahihi mwanzoni.
Endelea, yaliyo sahihi yako mbele na hutayafikia bila kupita kwa yasiyo sahihi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu usiwe mtu wa kujaribu na kuacha, bali fanya mpaka upate, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/05/2166

Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.