“Man needs difficulties. They are necessary for health.” – Carl Jung
Huwa hatupendi kukutana na magumu kwenye maisha,
Lakini magumu hayo ni muhimu sana kwetu,
Kwa sababu ndiyo yanayotuimarisha.
Mti unaoota eneo ambalo ni gumu, hakuna maji, kuna upepo mkali huwa unakuwa mti imara kuliko unaoota eneo lenye maji mengi na lisilo na upepo.
Kadhalika mwili huwa unatengeneza kinga pale unapokabiliwa na ugonjwa.
Yote hiyo ni mifano ya asili ya jinsi magumu yalivyo na manufaa kwenye maisha ya kila kiumbe.
Kama unataka mambo yawe rahisi tu, huwezi kufanikiwa.
Angalia hatua zote kubwa ambazo umewahi kupiga kwenye maisha yako, ni baada ya kukutana na ugumu fulani.
Hivyo usikimbie ugumu kwenye maisha yako,
Na unapokutana na ugumu, ukaribishe, angalia ni namna gani unakufanya kuwa bora zaidi.
Wale wanaokwepa ugumu, wanajiandaa mwenda kwenye anguko kubwa maana hawajijengi kuwa imara.
Wewe kabiliana na kila ugumu ili kuwa imara zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu wakati mambo yanapokuwa magumu, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/06/2167
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Hakika kocha maneno yanasadifu maisha halisi niliyoyapitia,ni kweli magunu yanatuimarisha na huo ndio ukweli
LikeLike
Vizuri.
LikeLike